CHAMA
Cha Mapinduzi Zanzibar kimesisitiza haja kwa Viongozi na Watendaji wake kuacha
tabia ya kuwabeba wana CCM wenye kutangaza nia ya kugombea nafasi za uongozi
katika Uchaguzi Mkuu wa dola ujao, kwani kufanya hivyo ni kukiuka kanuni na
miongozo ya Chama hicho.
Katibu
wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya
itikadi na Uenezi (Z) Bibi Waride Bakari Jabu, ametoa kauli hiyo wakati
alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Matawi na Wadi za Jimbo la
Dole, Wilaya ya Kichama ya Mfenesini.
Amesema
CCM inaongozwa kwa kanuni na taratibu zinazotambulika Kikatiba, hivyo
hakitomvumilia mwanachama yeyote anayevunja
kanuni hizo kwa maslahi yake binafsi kwani kila jambo limewekewa
utaratibu wake ambao unapaswa kufuatwa na kila Mwana CCM.
Amesema
ni marufuku kwa mwana CCM kuanza kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote hasa Ubunge, Uwakilishi au Udiwani, kwani muda wa kufanya hivyo bado haujawadia.
Ametoa
wito kwa Viongozi hao wa Jimbo la Dole la Wilaya ya kichama ya Mfenesini kuelekeza
nguvu zaidi katika kubuni mbinu na mikakati madhubuti kwa kuwaandaa watu wenye sifa za kupiga kura, ili
waweze kuleta ushindi wa kishondo wa Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Dola
wa Oktoba, mwaka huu (2015).
Nao,
Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Matawi na Wadi za Jimbo la Dole, wamesisitiza haja
ya kuendeleza suala zima la umoja na mshikamano miongoni mwao, kwa maslahi ya Chama
na Taifa kwa ujumla.
Katibu
huyo wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi, tayari ameshafanya
ziara katika majimbo ya 19 ya Mikoa ya Kichama ya Kaskazini, Kusini na Magharibi,
Unguja.
Imetolewa
na :-
Idara ya Itikadi na Uenezi - CCM,
ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇