Na Mwandishi Maalum, New York
Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake ( CSW) umeingia wiki ya pili ambapo wajumbe wameendelea kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu mada mbalimbali zinazohusu hadhi ya mwanamke na mtoto wa kike.
Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake ( CSW) umeingia wiki ya pili ambapo wajumbe wameendelea kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu mada mbalimbali zinazohusu hadhi ya mwanamke na mtoto wa kike.
Jana Jumatatu miongoni mwa majadiliano ambayo yamevutia wajumbe wengi yalihusu wajibu wa wanaume na wavulana katika kufikia usawa wa kijinsia.
Katika majadiliano hayo ilielezwa kwamba ili kufikia usawa wa kijinsia, basi hapana budi kuhakikisha kwamba wanaume na wanavulana wanashirikishwa kikamilifu katika safari hiyo.
Imeelezwa katika majadilianao hayo kuwa Ushiriki wa wanaume na wavulana kutaongeza kasi ya kufikiwa kwa usawa wa kijinsia, na kwamba jukumu hilo haliwezi likawa la wanawake peke yao.
Baadhi ya nchi zilichangia uzoefu wao wa namna gani zinatekeleza dhana hiyo ya kuhakikisha kwamba wanaume na wavulana wanatimiza wajibu wao kwa kuhakikisha kwamba jamii yote inakuwa na uelewa na ushiriki sawa katika kufikia lengo la kuwa na usawa wa jinsia.
Pamoja na majadiliano kuhusu mada hiyo, wajumbe wanaoshiriki mkutano huu pia wameendelea na majadiliano ya mada nyingine nyingi zilizokuwa zinafanyika katika kumbi mbalimbali za mikutano hapa Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya mada hizo ni ile iliyohusu : kubadlisha kanuni za jamii, ili kufikia usawa wa kijinsia, matarajio na fursa.
Ajenda kuu ya Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu hadhi ya wanawake, unaohudhuriwa na wajumbe kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Taasisi za UM na wawakilishi kutoka Asasi Zisizo za Kiserikali, ni Azimio la Beijing na Jukwaa la utekelezaji, miaka 20 baada ya kufanyika mkutano wa nne wa kihistoria wa wanawake, mkutano uliofanyika mwaka 1995 Beijing, China.
Kupia Ajenda hiyo ya Beijing+20) wajumbe wanajadili changamoto za utekelezaji wake na mafanikio katika usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.
Wajumbe pia wanajadili matokeo ya kikao maalum cha 23 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, tathmini ya miaka mitano baada ya kupitishwa kwa jukwa la utekelezaji, tathmini iliyoainisha hatua Zaidi na mipango inayotakiwa kutekelezwa ili kufika lengo la usawa wa kijinsia na uwezeshaji.
Vile vile mkutano huu unajadili fursa kwaajili ya kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji kupitia ajenda mpya za maendeleo baada ya 2015.
Mawaziri Mhe. Zainabu Omar Mohammed, kutoka Serikali ya Mapunduzi Zanzibar na Mhe Sophia Simba kutoka Serikali ya Muungano wakiwa na mwenyeji wao Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇