LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 3, 2015

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA KAPTENI JOHN KOMBA KIJIJINI KWAKE LITUHI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda  pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Tanzania kwenda kumzika marehemu Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi.

 Mke wa Marehemu Kapteni John Komba ,Salome (kushoto) akiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu.
 Watoto wa marehemu Kapteni John Komba wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba yao.
 Watoto wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati wa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Baba yao .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyezikwa kwenye makaburi ya kijiji cha Lituhi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Komba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Damian Komba aliyezikwa kijijini kwake Lituhi.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Lameck Mchemba pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyefariki jijini Dar es Salaam tarehe 28 februari na kuzikwa kijijini kwake Lituhi tarehe 3 Machi 2015.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu (kulia) akiweka shada la maua pamoja na mkewe kwenye kaburi la Kapteni John Komba.
 
Khadija Kopa akiwa katika huzuni kubwa mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages