Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wananchi wa Mpwapwa mjini na kuwaambia katika uongozi wake atawapa nafasi wale watu wanaotakiwa na wananchi wenyewe kuwaongoza na kusema hakutokuwa na makosa ya kukata majina.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa akiwahutubia wananchi wa Mpwapwa mkoani Dodoma na kuwaambi wawe makini na baadhi ya vyama vya siasa vinavyo andaa vijana kuingia msituni.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mpwapwa mkoani Dodoma kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mnarani.
Mkazi wa kata ya Lupeta wilayani Mpwapwa Gloria Manihuzi akiwakilisha kilio chao cha muda mrefu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (hayumo pichani) cha matatizo ya mawasiliano katika kijiji chao na kusisitiza kunahitajika juhudi za haraka zifanyike wapate mnara wa simu.
Mwalimu Mstaafu Silvanus Hosea akitoa maoni yake wakati wa mkutano wa hadhara kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alisema viongozi wa CCM hasa wanaogombea nafasi za uongozi wasipende kutoa ahadi zisizotekelezeka kwani zinachangia kupoteza imani ya wananchi kwa chama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamba la karanga la Bi. Anna Mlewa, wengine ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Chiku Galawa (kulia).
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubiawakazi wa Kisokwe kabla ya kushiriki ujenzi wa Zahanati.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea tofali kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa wakati wa kushiriki ujenzi ya zahanati ya Kisokwe.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Chiku Galawa akishiriki ujenzi wa zahanati ya Kisokwe .
Bweni lililoungua moto la shule ya sekondari Mpwapwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi lililoungua moto mapema mwanzoni mwa mwaka.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mpwapwa wakifurahia kusalimiana na Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kutembelea bweni la wanafunzi lililoungua moto.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇