WAZIRI wa Ujenzi Dk. John Magufuli ameagiza kufungwa kwa
mfumo mpya wa kielektroniki katika vivuko vyote nchini ili kukabiana na wajanja
wachache wanahujumu mapato katika vivuko hivyo.
Mbali ya hilo,
ameagiza kufanywa kwa utaratibu utakaowezesha huduma katika vivuko zinatolewa
kwa saa 24 ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
Dk. Magufuli alitoa maagizo hayo jana katika uzinduzi wa
mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa
uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
"Tulianze pale Kigamboni na tukaona mafanikio,
tulipokuja hapa (Kigongo) tukaboresha na mafanikio yameonekana kwa kiasi
kikubwa. Vivuko vyote sasa vifungwe mfumo mpya wa kielektroniki...vivuko vyote
nchini," aliagiza Magufuli.
Alisema mfumo huo una faida kubwa ikiwemo kudhibiti upotevu
wa mapato ambapo katika kivuko cha kigongo - Busisi alisema mapato yameongezeka
kwa takribani asilimia 40 baada ya kufungwa kwa mfumo huo.
Hata hivyo, Dk. Magufuli alikataa kutaja ni kwa shilingi
ngapi mapato hayo yameongezeka kwa hofu kuwa watu wenye dhmira mbaya wakisikia
wanaweza kwenda na kufanya uhalifu.
Pia, aliagiza Kivuko kwa Kigamboni nacho kiboreshwe mfumo
wake kama ilivyokuwa kwa Kigongo -
Busisi.
Waziri huyo wa Ujenzi, alisema kutokana na mafanikio yanayopatikana
katika kudhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi,
wafanyakazi husika kwa maana ya wale wa TEMESA maslahi yao yanapaswa kuangaliwa upya na kuboreshwa.
"Kama mapato ni mazuri, wafanyakazi nao walipwe vizuri,
wasikae kimasikini kwani wanapaswa kuona mwaka 2015 ni ukombozi katika maisha yao.
Alisema serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete
imefanikiwa kujenga madaraja yote makubwa nchini ambapo kwa sasa kuna madaraja
4880 nchini na kuwa wakati inapata uhuru kulikuwa na madaraja mawili ambayo
yalikuwa ya kuvutwa.
Mfumo wa kielektroniki katika vivuko vya Kigamboni na
Kigongo Busisi ulifungwa na Kampuni ya Africom Tanzania ambaye Mkurugenzi Mtendaji
wake Juma Rajabu alisema watahakikisha wanafunga mifumo ambayo itadhibiti
upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi ambao ndiyo watumiaji.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇