Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alipokuwa anazungumzia maazimio ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika Zanzibar tarehe 13 Januari 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Jana
tarehe 13/01/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya
uongozi wa Mwenyekiti wake wa Taifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilifanya
kikao chake cha kawaida cha siku moja Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni pamoja na:-
1. SAKATA LA AKAUNTI YA ESCROW
Chama
Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na sakata hili. Baada ya kulijadili
kwa muda mrefu na kwa kina Kamati Kuu imeamua yafuatayo:-,
i).
Pamoja na yale ambayo yameshatekelezwa na serikali, Kamati Kuu imeitaka
serikali na vyombo vinavyohusika kuendelea kutekeleza maazimio ya bunge
juu ya swala hilo.
ii). Kamati Kuu imewataka
wote wanaopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika kwa dhamana zao,
na wasipowajibika waliowapa dhamana wachukue hatua za kuwawajibisha.
iii).
Aidha Kamati Kuu imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuchukua hatua za
kimaadili kwa wale wote waliohusika na ukiukwaji wa maadili kwenye
sakata la Escrow na wako kwenye vikao vya maamuzi vya Chama. Kikao cha
Kamati Ndogo ya Maadili kitafanyika tarehe 19/01/2015 kwa ajili ya
utekelezaji wa agizo hilo.
2. WALIOPEWA ADHABU KWA KUKIUKA MAADILI YA CHAMA.
Itakumbukwa
kuna makada sita wa CCM walipewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa
maadili kwenye mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais,
watamaliza muda wa adhabu zao mwezi wa pili mwaka 2015.
Baada
ya muda wa adhabu zao kuisha, itafanyika tathimini kuona kama
walizingatia mashariti ya adhabu zao. Na kama kuna ambao watakutwa
hawakuzingatia mashariti ya adhabu zao wataongezewa adhabu.
3. SOKO LA MAHINDI
Kamati
Kuu imepokea taarifa ya mwenendo wa soko la mahindi nchini. Baada ya
tathimini na uchambuzi, pamoja na kazi iliyofanywa na serikali, Kamati
Kuu imeiagiza serikali kuangalia upya mfumo unaotumiwa na Hifadhi ya
Taifa ya Chakula ( NFRA)katika ununuzi wa mahindi, ili unufaishe zaidi
wakulima badala ya utaratibu wa sasa ambao kwa kiasi kikubwa unanufaisha
zaidi mawakala badala ya wakulima moja kwa moja.
4. RATIBA YA VIKAO VYA CHAMA.
Kamati Kuu imepitisha ratiba ya shughuli mbalimbali za Chama kwa mwaka 2015.
Aidha ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM ndani ya dola utapangwa na vikao vijavyo vya Chama.
Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇