Na Emanuel Madafa,Mbeya,
Jumla ya 1486 wa masomo ya
sayansi na hisabati kati ya 2614 wanahitajika mkoani Mbeya i kukidhi mahitaji
ya shule zote za sekondari za serikali zilizomo ndani ya Mkoa wa Mbeya.
Akizungumzai changamoto
hiyo , Katibu Tawala wa Mkoa wa
Mbeya, Mariam Mtunguja, amesema idadi hiyo inatokana na takwimu za mwaka 2013.
Amesema, uhitaji wa walimu kwa Mkoa wa Mbeya ni 2614 lakini
waliopo ni 1128 pungufu ni walimu 1486 sawa na asilimia 57.
Amesema, kwa upande wa halmashauri mbili likiwemo Jiji la Mbeya na
Mbeya vijijini jumla ya walimu 342 wa masomo hayo wanahitajika.
Amesema kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya pekee ,
inawalimu 237 upungufu ni walimu 255 na wanaohitajika ni 1996 huku
halmashauri ya Mbeya inauhitaji wa walimu 751 waliopo ni 129 upungufu ni walimu
77,”alisema.
Amesema, serikali imekuwa ikijitahidi kuzalisha idadi
kubwa ya walimu wa masomo hayo lakini bado changamoto hiyo ni kubwa na hali
hiyo inachangiwa na wanafunzi kuyakimbia masomo hayo pamoja na
ukosefu wa vyuo vya ualimu.
Amesema, jambo muhimu linalopaswa kutekelezwa na wazazi
au walezi wa watoto ni kuwahamasisha vijana kupenda kusoma masomo ya sayansi
kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza tatizo hili la uhaba wa
walimu.
Halmashauri ya Busokelo inaupungufu wa walimu wa sayansi na
hisabati kwa asilimia 65,Chunya asilimia 42,Ileje asilimia 63, Kyela asilimia
68, Mbarali asilimia 67, Jiji asilimia 56, Mbeya vijijini asilimia 45, Mbozi
asilimia 75, Momba asilimia 65 na Rungwe asilimia 30.
Mwisho.
JAMIIMOJABLOG
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇