TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI.
Jumuiya
ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) inampongeza
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba
yake nzuri iliyojaa ufafanuzi bayana wa masuala makubwa ya kitaifa,
likiwemo suala la Akaunti ya Escrow ya Tegeta, yaliyoleta mkanganyiko
kwa wananchi, aliyoitoa jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee
alipozungumza na wazee wa jiji la Dar es salaam.
Sisi
Vijana tunampongeza kwa kubariki na kuridhia hatua iliyochukuliwa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, Mheshimiwa Hawa Ghasia za kuwachukulia hatua sitahiki
wakurugenzi wazembe waliovuruga Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka
huu.
Tunahimiza
utaratibu huo uwe endelevu kwa kuendelea kuwachukulia hatua kali
wakurugenzi ambao wanapata hati chafu za Ukaguzi pamoja na wale ambao
wanashindwa kutimiza wajibu wa kisheria wa kutenga asilimia tano (5)
za mapato ya Halmashauri kwa ajili ya maendeleo ya Vijana.
Pia,
Tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri
wa Ardhi, (Mb) Mheshimiwa Anna Kajumulo Tibaijuka.
Tunamwomba
Mheshimiwa Rais kumteua Waziri mwingine ambaye atamudu wizara hiyo
ipasavyo kwa kutatua na kumaliza kabisa migogoro ya ardhi ambayo
imeendelea kusababisha vurugu, machafuko na maafa katika maeneo
mbalimbali hapa nchini kama vile Mvomero, Maswa, Kiteto.
Tunapendekeza apatikane Waziri ambae muda wake mwingi atakuwa katika
maeneo hayo akitafuta suluhu ya kudumu kati ya wafugaji na wakulima,
baina ya wafugaji, wakulima na hifadhi, na baina ya wananchi, hifadhi
na wawekezaji.
Pia,
tunavitaka vyombo vinavyoendelea na uchunguzi, kumaliza na kukabidhi
matokeo ya uchunguzi wao katika mamlaka husika mapema ili kutoa fursa
kwa maamuzi kufanyika kwa wakati.
Tunavitaka
vyombo hivyo kufanya kazi zake kwa weledi na uaminifu mkubwa ili
jambo hili lipate maamuzi sahihi lakini pia asionewe mtu na haki
itendeke.
Na
mwisho tungependa kuwakumbusha wananchi na viongozi kuheshima
mgawanyo wa madaraka, na kuheshimu nguvu na mamlaka za kila mhimili
wa Taifa, tunaiomba Mamlaka ya Bunge iendelee na utaratibu wake
katika kuwashughulikia wale walio kwenye mamlaka zake ambao
wamehusika katika kadhia hii ya ESCROW na pia kuitaka mahakama na
tume zake kuchukua hatua kulingana na taratibu na miongozo yao.
Tunawaomba
Wananchi kuwa makini na kutoruhusu mijadala inayohusu suala hili
kutawaliwa na maslahi binafsi ya wafanyabiashara na wanasiasa, ambao
wameendelea kushawishi na kushinikiza maamuzi yanayolinda maslahi
yao.
Imetolewa
na:-
Paul
Makonda
Katibu,
Idara ya Hamasa na Chipukizi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇