LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 28, 2014

SERIKALI YAENDELEA KUPAMBANA NA NJIA ZA PANYA MPAKA WA TUNDUMA WADAU NAO WATOA USHAURI


 Kaimu afisa wa  Idara ya Forodha, Majaliwa Omary





Bidhaa zilizokamatwa katika baadhi ya Bar Mjini Tunduma ambazo zimeingia nchini kinyume cha taratibu kupitia njia za Panya.


Afisa ukaguzi wa mamlaka ya Chakula na Dawa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Yusto Wallace
Meneja biashara  wa kinywaji  cha Bear aina ya , Wind hock Ndugu Joseph Boniface,akionyesha utofauti kati ya Bear inayosambazwa na Mabibo Bea kutoka Dar es salaam na ile inayoingizwa nchini kutoka sauth afrika kinyume cha taratibu kupitia njia za panya.



Hii ni halali kwa soko la Tanzania ambayo ina nembo ya Mabibo Beer  kutoka Namibia
Hii si halali kwa soko la Tanzania ikiingizwa nchini kupitia njia za Panya ikitoke nchini Sauth Afrika

Na EmanuelMadafa,Tunduma
Kwa kiwango kikubwa serikali imekuwa ikipoteza kiasi kikubwa cha fedha  kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya njia za panya zinazotumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa  kupitishia bidhaa za magendo katika maeneo ya mipakani.

Hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakitekeleza sheria za ulipaji wa kodi, kushindwa kuendesha biashara hizo kutokana na uwepo wa bidhaa zinazoingizwa kwa njia ya magendo sokoni.

Akizungumza na waandishi wa habaari, Meneja biashara  wa kinywaji  cha Bear aina ya , Wind hock Ndugu Joseph Boniface, amesema serikali inatakiwa kudhibiti njia zote za panya ambazo zinatumiwa na wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa zao kwa njia ya magendo ili kutenda haki kwa wale wanaochangia pato la taifa kwa kulipa kodi.

Amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo serikali bado itaendelea kupoteza kiasi kukubwa cha fedha pamoja na kuongeza bidhaa ambazo ubora wake haukidhi soko la ndani.

Amebainisha kuwa yapo baadhi ya maeneo ambayo katika mji huo wa tunduma hususani  kwa baadhi ya bar na hotel zimekuwa zikuza bidhaa hiyo ya    Bear ya Wind hock ambayo imeingizwa nchini kinyume cha sheria ikitokea Afrika ya Kusini na kuingia Tanzania kwa njia ya panya kwa kupitia mpaka wa Tunduma.

Akizungumzia changamoto hiyo  Kaimu afisa wa  Idara ya Forodha, Majaliwa Omary   alisemaa  ni ngumu kudhibiti magendo kutokana na hali  ya uwazi na njia za panya zilizokithiri ndani ya mpaka huo.

Amesema,  kutokana na mianya hiyo magari yamekuwa yakipitisha bidhaa halamu na halali kwa kutumia njia za panya na kuingia upande wa pili wa mpaka ama kuingiza nchini pasipo vikwazo hali ambayo imechangia pia udhibiti mdogo wa bidhaa kama dawa, vyakula na vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku.

Naye Afisa ukaguzi wa mamlaka ya Chakula na Dawa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Yusto Wallace, aliitaka jamii kujenga utamaduni wa kutumia bidhaa ambazo zimekaguliwa na mamlaka  za udhibiti.

Aidha,aliiomba serikali kuijengea uwezo TFDA hasa katika kuajiri watumishi wanaokidhi mahitaji ya udhibiti ili kukabiliana na ongezeko kubwa la wafanyabiashara ambao wanaendesha shughuli zao kinyume cha utaratibu.

Hata hivyo,amesema TFDA imeweza kukamata shehena ya vinywaji mbalimba ambavyo vimeingizwa nchini kinyume cha utaratibu na zilizomaliza muda wake wa kutumika ikiwemo Bear aina ya Wind Hock ya kutoka Afrika ya Kusini.JAMIIMOJABLOG

Mwisho.



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages