DAR ES SALAAM, Tanzania
MKE
wa mlalamikaji katika kesi ya kughushi dhidi ya Mfanyabiashara Hans
Macha (pichani), amedai mahakamani kwamba mumewe anadaiwa fedha nyingi
na mshtakiwa, alishindwa kulipa akaamua kumuuzia nyumba.
Mke
huyo Nurya Ahmad (34),ambaye ni shahidi wa upande wa utetezi, amedai
hayo leo Desemba Mosi, katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu,Dar es
Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, kwa kuongozwa na wakili wa
utetezi, Deo Ringia.
Nurya amedai mahakamani hapo kwamba nyumba
iliyokuwa ya Balenga iliyopo eneo la Kigogo, Dar es Salaam, iliuzwa
kihalali kwa Macha baada ya mumewe (Balenga), kushindwa kulipa deni.
“Nafahamu
kwamba mume wangu (Balenga), alikuwa andaiwa na Macha, aliniambia
mwenyewe kwamba ni fedha nyingi sana, deni halikuwahi kulipwa hatimaye
akaniambia kuwa ameeamua kumuuizia nyumba.
“Alikuwa akikopa kwa
kuweka rehani hati za nyumba, madeni mengine yalikuwa yakilipwa,
tulikuwa katika ndoa kuanzia mwaka 2001 hadi 2012, sijawahi kuona mume
wangu akiwa kichaa,” alidai Nurya baada ya kuulizwa kama aliwahi kuona
mumewe akiwa kichaa.
Shahidi huyo alihoji mahakamani kwamba hati
za nyumba halisi zilifikaje kwa Hans Macha, kama Balenga hakuzipeleka
mwenyewe kwake, aliongeza kwamba hajawahi kumsikia mumewe akilalamika
kudhulumiwa nyumba na Macha.
Mfanyabiashara
Hans Macha akijitetea alidai kwamba Ramadhani Balenga alishindwa
kumlipa deni la Sh. milioni 879 akamuuzia nyumba iyo ya Kigogo.
Alidai
Balengo alikuwa akimtegemea kwa kukopa fedha mara kwa mara kwa ajili ya
kuingiza makontena ya vifaa vya umeme au elektroniki.
“Aliletwa
na wafanyabiashara wenzangu kwa ajili ya kukopa, nilimpa masharti ya
kukopa, aliweka dhamana hati ya nyumba yake ya Mabibo, Manzese, Kigogo,
Mbezi Beach, mara ya mwisho Balenga nilikuwa namdai jumla ya Sh. milioni
879, wakati huo nilikuwa na hati zake za nyumba nne.
“Balenga
alishindwa kulipa akidai kwamba kontena zake zilikamatwa na kufilisiwa
na TRA, aliamua kuniuzia nyumba ya Kigogo, Manzese na nimuongezee Sh.
milioni 20 ili tumalizane deni lote.
“Nilipofanya hivyo mbele ya
wakili nilikuwa nimempa jumla ya Sh. ilioni 899, nilipomkabidhi fedha ya
nyongeza Sh. milioni 20 alinikabidhi hati, siku nyingine tulisaini hati
ya kuhamisha umiliki,
Balenga alinikabidhi nyaraka zingine
ikiwemo michoro, mikataba ya ujenzi, kibali cha ujenzi, miakataba halisi
waliyoingia na kampuni ya ujenzi pamoja na risiti mbalimbali,” Macha
alidai.
“Si kweli kwamba nilighushi, Balengo aliniuzia nyumba
baada ya kushindwa kulipa deni, naiomba mahakama iyatupe mashtaka
yaliyofunguliwa dhidi yangu,”alidai Macha.
Shahidi wa tatu,
Mohammed Waziri Mohammed ambaye ni mfanyakazi wa Balenga pia alidai
mahakamani kwamba mlalamikaji katika kesi hiyo alikuwa akidaiwa na
Macha.
Waziri alidai mara kadhaa alikuwa akienda na mlalamikaji
kwa Macha kwa ajili ya kukopa fedha. Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea
kesho Jumanne, Desemba 2, 2014
Your Ad Spot
Dec 1, 2014
Home
Unlabelled
MKE AKIRI MUMEWE BWANA BALENGA KUUZA NYUMBA KWA MFANYABIASHARA HANS MACHA KUTOKANA NA MFANYABIASHARA HUYO KUMDAI MAMILIONI YA FEDHA
MKE AKIRI MUMEWE BWANA BALENGA KUUZA NYUMBA KWA MFANYABIASHARA HANS MACHA KUTOKANA NA MFANYABIASHARA HUYO KUMDAI MAMILIONI YA FEDHA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇