Mbunge wa jimbo la mufindi wa kasikazini ambaye pia naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa
Mbunge
wa jimbo la mufindi wa kasikazini ambaye pia naibu waziri wa maliasili
na utalii Mahmoud Mgimwa akiwa na mkuu wa wilaya wa mufindi.
Mbunge wa jimbo la mufindi wa kasikazini ambaye pia naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa akiwa amevalia
Na fredy mgunda Iringa.
Vijiji
31 vilivyopo mufundi kaskazini mkoani Iringa vinatarajia kupokea umeme
na tayari baadhi ya vijiji vipo katika hatua ya mwisho ya kufunga
vikombe kwaajili ya kuanza kuvuta nyaya.
Akizungumza
na mwandishi wetu katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini ambae
pia ni naibu waziri wa maliasili na utalii Babtist Mdende amesema kuwa,
vijiji vinavyotarajia kupata umeme safari hii ni vile vijiji vilivyopo
tarafa ya sadani,ifwagi na kibengu.
“vijiji
hivyo ni mapogoro, igomaa,kibada,ndolezi na vengine kama
ugesa,vikula,ilasa na kipanga ambavyo upimaji bado unaendelea kwaajili
ya kusimika nguzo,
“kunabaadhi
ya vijiji vipo katika hatua ya awali ya kusimamisha nguzo ikiwepo
kijiji cha Isalavanu ambacho mradi wake wa umeme unashughulikiwa na
TANESCO wilaya ya mufindi”, alisema Mdende.
Aidha
Mdende ameeleza kuwa kwa wale watakao ingazwa kwa mara ya kwanza yaani
watu wa kwanza wakati wa kuzindua mladi wa umeme wataingiziwa kwa
gharama ya shilingi elfu 30
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇