Na Emanuel Madafa,mbeya
Chama
cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya kikiendelea kupata ushindi katika matokeo ya
awali katika uchaguzi wa serikali za mitaa huku vyama vya upinzani vikifuata
kwa mbali
Kwa
mujibu wa matokeo ya awali yaliyotelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Mwangi
Kundya, yanaonesha kuwa, chama hicho kimefanikiwa kuzoa idadi kubwa ya vijiji
hadi sasa.
Akitangaza
matokeo hayo mbele ya waandishi wa habariKundya amesema matokeo ya awali katika
Halmashauri ya Jiji la Mbeya lenye mitaa 181, CCM imefanikiwa kupata mitaa 106,
Chadema71, NCCR-Mageuzi mmoja.
Wilaya
ya Chunya yenye Vijiji 86,ambapo vijiji vilivyokamilisha hesabu ni 74, CCM
ilipata vijiji 67 , Chadema vijiji 7, wakati kwa upande wa vitongoji, CCM
ilipata vitongoji 270, huku Chadema ikiambulia vitongoji 18.
Wilaya
ya Ileje jumla ya vijiji vyote ni 71 ambapo vijiji 32 vimekamilisha matokeo
yake, ambapo CCM imepata vijiji 23, Chadema vijiji 9, ambapo kwa upande wa
vitongo….
Wilaya
ya Kyela vijiji vyote 93 vimekamilisha matokeo yake, ambapo CCM imepata
79,Chadema 13 , huku uchaguzi wa kijiji kimoja kurudiwa ambapo kwa upande wa
vitongoji 469, CCM vitongoji 377, Chadema 88, wakati vitongoji vine uchaguzi kurudiwa.
Wilaya
ya Mbarali jumla ya vijiji 102, CCM 81,Chadema 16 ambapo vijiji sita vitafanya
uchaguzi wa marudio, ambapo kwa upande wa vitongoji jumla ni 713, ambapo CCM
imeshinda vitongoji 570 , Chadema ikiambulia 79 na vitongoji 36 matokeo yake
yalikuwa bado.
Wilaya
ya Mbozi, vijiji vilivyopo ni 125 ambapo kati ya hivyo 92 matokeo yake yalikuwa
tayari ambapo CCM imepata viti 84 na Chadema imepata vijiji nane, huku vijiji
33 matokeo yalikuwa bado, kwa upande wa vitongoji 664, CCM imepata 557 na
Chadema 110, CUF viwili,TLP ikiambulia kiti kimoja.
Wilaya
Rungwe jumla ya vijiji 155 , CCM imepata 132,Chadema 22, CUF kimoja na vijiji
vitano kufanya marudio, wakati upande wa vitongoji vilivyopo ni 694,CCM
578,Chadema 111,CUF 2 na TLP viwili.
Wilaya
ya Momba ambayo matokeo yake yamegawanywa katika sehemu mbili kutokana na
wilaya kuwa na Halmashauri ya mji wa Tunduma.
Ambapo
kwa upande wa vijiji jumla ni 72, CCM imepata vijiji 43,Chadema24 na vijiji
vitano kufanyiwa marudio, wakati kwa upande wa vitongoji, jumla ni vitongoji
302, CCM 189, Chadema 53 na vitongoji 60 matokeo yake bado.
Kwa
upande wa mitaa katika Halmashauri ya mji wa Tunduma jumla ya mitaa ni 71, CCM
imechukua mitaa 25, wakati Chadema imeongoza kwa kupata mitaa 46, hivyo
kulazimika kuunda Halmashauri ya mji.
Wakati
matokeo ya Wilaya hizo yakipatikana katika mkoa wa Mbeya kwa upande wa Wilaya
ya Mbeya Vijijini matokeo ya awali yameshindwa kutolewa kutokana na utata wa
hesabu, lakini pia Jografia ya wilaya hiyo kuwa na changamoto ya mpangilio
wake.
Hata
hivyo, habari za uhakika zinadai kuwa katika uchaguzi wa mamlaka ya mji
Mbalizi, CCM imepata vitongoji viwili, huku chadema ikipata vitongoji 10 kati
ya 12 hivyo kuwa na uhakika wa kuunda baraza la mamlaka ya mji.
Ndugu CEO wa blog hii jaribu kuandika kitu sahihi ili wananchi wajue ukweli na kitu kilichojili na uache ushabiki. Naomba ufuatilie vizuri taarifa yako na usitupotoshe.
ReplyDelete