LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 16, 2014

ZIARA YA KINANA YAANZA VIZURI MKOANI LINDI

 Umati wa wakazi wa Chumo waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndugu Abdala Ulega akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa CCM kata ya Tingi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  wakati akiwasili kwenye kata hiyo tayari kushiriki ujenzi wa ofisi ya Kijiji.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama Mheshimiwa Bernard Membe akisalimia wakazi wa kata ya Tingi
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nappe Nnauye akiwasalimu wakazi wa kata ya Tingi waliojitokeza kushiriki ujenzi wa ofisi ya kijiji .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa kata ya Tingi kabla ya kushiriki ujenzi wa ofisi ya kijiji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya kijiji Tingi.
 Mheshimiwa Membe akimsikiliza mmoja wa wananchi wa Tingi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma vijiviji vitkavyopatiwa umeme kwenye mradi wa umeme vijiji unaonedele kwa wananchi wa kata ya Chumo.


  Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Bernard Membe akiwasalimia wananchi wa kata ya Chumo.

  Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Bernard Membe akiingia kwenye uwanja wa mikutano huku akicheza muziki wa chama pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndugu Abdala Ulega na wananchi  wa kijiji cha Chumo kwenye uwanja wa shule ya msingi Chumo.
 Umati wa wakazi wa kata ya Chumo wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Wananchi wa Chumo wamepewa sifa ya utulivu kwenye mikutano yao.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilwa ndugu Abdala Ulega akiwasalimu wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya shule ya msingi Chumo kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Maimuna Mtanda akiwasalimu wakazi wa kata ya Chumo
 Mbunge wa Viti Maalum Fatuma Mikidadi akiwasalimia wananchi wa kata ya Chumo waliojitokeza kwa wingi kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Bernard Membe akiwasalimia wananchi wa kata ya Chumo waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM alihutubia ikiwa ndio siku ya kwanza ya ziara yake ya siku 16.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Chumo kwenye viwanja vya shule ya msingi Chumo na kuwaambia kuwa huu si muda tena wa kuwasikiliza wapinzani kwani upinzani ulishaisha nchini hivyo .
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa akitoa salaam za kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Chumo kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chumo ikiwa siku ya kwanza ya kuanza ziara yake ya mikoa miwili ya Lindi na Mtwara.
 Wananchi wakifuatilia mkutano kwa makini
 Wazee wakifuatilia  mkutano
 Wazee wa Chumo wakifuatilia mkutano

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Kata ya Chumo ambapo aliwaambia CCM ni chama pekee chenye mfumo unaoeleweka wa uongozi unaofuata demokrasia ya ukweli hivyo basi aliwata wananchi hao kushikamana na CCM


 Wazee wakiwa makini mkutanoni
 Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini Ndugu Multazar Ally Mangungu akiwahutubia wakazi wa kay ya Chumo ambapo aliwaelezea mipango mbali mbali inayokaribia kukamilika ikiwa pamoja na kuondoa tatizo sugu la mawasiliano ya simu kwa wakazi hao.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahim Kinana akionyesha kadi ya Chama cha Chadema iliyorudishwa na Bwana Mohamed Hassan wa kijiji cha Chumo
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahim Kinana akimkabidhi kadi ya uanachama wa CCM Bwana Mohamed Hassan wa kijiji cha Chumo ambaye amejiunga na CCM kutoka Chadema.
 Wananchi wakiburudika baada ya mkutano kumalizika.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akpongezwa na Mbunge wa Mtama na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  Ndugu Bernard Membe pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilwa .

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages