Hali
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ambaye alifanyiwa operesheni Jumamosi, inaendelea kuimarisha
na kuwa nzuri na jana, Jumapili, Novemba 9, 2014, alianza kufanya
mazoezi ya kutembea.
Rais
Kikwete ameanza kufanya mazoezi ya kutembea siku ya pili tu baada ya
kufanyiwa operesheni ya tezi dume (prostrate) kwenye Hospitali ya
Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Maryland, Marekani.
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, itaendelea kuwapatia wananchi habari
sahihi kuhusu maendeleo ya afya ya Mheshimiwa Kikwete kwa kadri
habari hizo zitakavyokuwa zinapatikana.
Aidha,
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kuwashukuru sana
wote ambao wamekuwa wakimwombea Rais Kikwete, ili apone haraka na
kurejea nyumbani kujiunga na wananchi wenzake katika ujenzi wa taifa
letu. Tunawaomba waendelee kumwombea.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇