NA BASHIR NKOROMO
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu
wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal ametoa mwito kwa viongozi na
wanachama wa chama hicho kuacha misuguano na mifarakano ili kukiepusha
mipasuko isiyo ya lazima.
Dk.
Bilal (pichani), ambaye pia ni mlezi wa Chama mkoa wa Dar es Salaam, alitoa mwito huo wakati akiwahutubia katika mkutano uliowakutananisha viongozi
mbalimbali wa chama hicho kuanzia ngazi ya chini wakiwemo wajumbe wa
Halmashauri Kuu za Wilaya na Mkoa kujadili uchaguzi wa Serikali za Mitaa
na Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Alisema
CCM ni chama pekee hapa nchini ambacho kinafanya shughuli zake
kidemokrasia na ndio maana kinaendelea kushika dola na kukubalika na
wananchi.
Dk.Bilal
alisema katika kipindi hiki cha mchakato wa kuwapata viongozi kuelekea
katika chaguzi mbalimbali kunakuwa na changamoto za hapa na pale hivyo
wenye dhamana ya kuwateua wagombea wanapaswa kutenda haki kwa kumteua
yule aliyepigiwa kura kwa wingi badala ya kufanya ndivyo sivyo.
"Chama
Cha Mapinduzi ndio chama chenye dira na sera zinazotambulika hivyo
viongozi wake wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha hakuna makundi
yanayoweza kuwagawa wanachama" alisema Bilal
Alisema
viongozi wa chama hicho wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha chama hicho
kinapata ushindi wa kishindo katika chaguzi zote kwani uwezo wa kufanya
hivyo upo kwa kuwa chama hicho kimejipanga vizuri kuanzia ngazi ya
shina na kina maadili.
Bilal
aliongeza kuwa kila uchaguzi unapofanyika watu na vyama vingine
wanaangalia CCM imemsimamisha nani hivyo ni vizuri wakati wa uteuzi wa
viongozi wanapaswa kuwa makini kwa kumchagua aliyebora.
Mwenyekiti
wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema
wamejifunza mengi katika chaguzi zilizopita ambapo walipoteza maeneo
kadhaa kwa kuchuliwa na vyama v, kwa sasa wako katika hatua za mwisho za
kupata mgingine kutokana na makosa hayo.
Alisema
hivi sasa mwanachama yeyote atakaye shinda kura za maoni ndiye
atakayekuwa mgombea katika eneo husika labda tu awe amepita kwa rushwa
na mambo mengine ambayo yatathibishwa.
Makamu wa Rais na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida wakiingia ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya mkutano. (Imeandaliwa na www. habari za jamii.com)
viongozi mbalimbali wa chama hicho kuanzia ngazi ya chini wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu za Wilaya na Mkoa wakimkaribisha mgeni rasmi wa mkutano huo, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Garib Bilal (hayupo pichani)
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba "Gadafi" akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, akihutubia kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dk. Bilal.
Makamu wa Rais ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mpinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Mohamed Gharib Bilal (katikati), akizungumza na viongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam leo, kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu 2015. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonah Kaluwa (katikati), akifurahia jambo na viongozi wenzake katika mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanaccm wakiwa wamefurika ukumbi wa Karimjee
katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanaccm wakiwa katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇