Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akimuonesha Rais Jakaya Kikwete (kulia) mchoro unaoonesha jinsi wakimbizi wa Burundi walivyoingia nchini wakati walipokuwa wanatoka nchini kwao mwaka 1972. Kuli kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza baada ya kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania, waliokuwa wakimbizi 162,156 kutoka nchini Burundi walioingia nchini tangu mwaka 1972.
Msoma risala ambaye ni mwakilishi wa raia wapya 162,156 nchini ambao walikuwa wakimbizi kutoka nchini Burundi, Dafroza Baragwimba akiisoma risala yao mbele ya Rais Jakaya Kikwete (watatu kulia) wakati ya hafla ya utoaji wa vyeti kwa raia hao.
Sehemu ya wakimbizi wa Burundi 162,156 ambao sasa ni raia wa Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwapa uraia.
Rais Jakaya Kikwete (wa sita kushoto waliokaa), mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wa tano kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa (wa sita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya raia wapya 162,156 wa Tanzania (nyuma waliosimama) baada ya kupewa vyeti vya uraia na Rais Kikwete
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇