Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza kikao cha
Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vilivyopigania Ukombozi wa Nchi Kusini
mwa Afrika (FLM). Kushoto kwa Kinana ni Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF
ya Zimbabwe Comrade Didymus Mutasa na anayefuata ni Katibu Mkuu wa ANC
ya Afrika Kusini Comrade Gwede Mantashe. Kulia kwa Kinana aliyevaa
miwani ni Katibu Mkuu wa MPLA ya Angola Comrade Juliao Mateus Paulo
'Dino Matrosse' na anayefuata ni Katibu Mkuu wa SWAPO Party ya Namibia
Comrade Nangolo Mbumba.
Mkutano huo wa siku moja umefanyika leo tarehe 10 Septemba, 2014 Jijini Johannesburg, Afrika Kusini na ulikuwa na ajenda Kuu ya Ujenzi wa Chuo cha pamoja cha Vyama kitakachojengwa Ihemi, Iringa Tanzania. Madhumuni ya Chuo hicho ni kubadilishana uzoefu na kurithisha historia ya Ukombozi kwa vizazi vijavyo.
(Imetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM)

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇