Na EmanuelMadafa,Mbeya
MAMLAKA ya udhibiti na
usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) inatarajia kubadilisha matumizi ya
mitimbwi ya kienyeji inayo tumika kusafirisha abiria kwenye bahari, maziwa na
mito kutokana na vyombo hivyo kukosa ubora na umathubuti hali inayohatarisha
usalama wa watu, vyombo na mali.
Akizungumza na Blogu hii kwenye maonyesho ya Sherehe za NaneNane Nyanda
za Juu Kusini yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale
vilivyopo eneo la Uyole Jijini Mbeya,Ofisa Udhibiti wa Majini, Adam Mamilo, amesema
mitumbwi mingi imejengwa kwa kienyeji tena kwa kutumia mbao ambazo si elekezi.
Alisema, mitumbwi hiyo
hutengenezwa kwa kutumia mbao ambazo hazikidhi viwango hali inayochangia
kupoteza uhai wake ambao upo kwenye wastani wa miaka 3 hadi 5 ukilinganisha na
miaka 35 kwa vyombo vilivyojengwa kwa viwango.
Amesema, kinachojitokeza
katika hali hiyo,ni kupungua kwa ubora na umathubuti wa vyombo hivyo
vinavyoundwa na kuhatarisha usalama wa watu, vyombo na mali.
Amesema, utafiti huo
ulibaini kuwa miundo na uundaji wa boti au mitumbwi inayotumika Tanzania ni ule
wa kutumia miti mikubwa na kuchimba umbile la chombo na unatumika kwa vyombo
vidogo kwenye baharini, maziwa na mtoni.
Amesema kuwa mitumbiwi
hiyo si salama kwa matumizi ya binadamu
kwani hutengenezwa kwa kutumia miti mikubwa ambayo huchimbwa umbile la chombo
na kutumika kwa vyombo vidogo baharini, mtoni na maziwa jambo ambalo limekuwa
hatari zaidi mara mawimbi yanapopiga kitendo ambacho kinahatarisha uhai wa
mtumiaji.
.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇