Baadhi
ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji toka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika
Utumishi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Hassan Silayo)
|
Na Georgina Misama
Serikali
imewataka waombaji kazi waliobadilisha majina, waliosoma nje ya Nchi, kupoteza,
kuibiwa, kuharibikiwa au kuunguliwa na vyeti kufuata taratibu pindi wanapoomba
kazi secretariati ya ajira.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Rais, Sekretariat ya
Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham wakati wa mkutano na waandishi
wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Riziki
alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko toka kwa waombaji wa kazi kuwa
secretariati ya Ajira imekuwa na upedeleo kwa kutowaita au kuwazuia
kufanya usaili waombaji wasiokuwa na
nyaraka halisi.
Riziki
alifafanua kuwa pindi waombaji wanapokabiliwa na hali hiyo hawana budi kutoa
tarifaa katika mamlaka husika ili taratibu za kupata vyeti vingine zifanyike na
taarifa zao kutumwa Secretariati ya Ajira kwa wakati.
Akizitaja
Mamlaka hizo Riziki alisema ni Polisi, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA),
Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Tume ya Vikuu (TCU), na Baraza la
Usimamizi wa Elimu ya Vyuo vya Ufundi (NACTE).
Aidha,
Riziki aliongeza kuwa kwa waombaji wenye majina tofauti kwenye vyeti wanapaswa
kwenda mahakamani na kula kiapo kwa kamishna wa viapo au kwa wakili ili waweze
kupata (Deedpal) au (Affidavity) kwa mujibu wa sheria na kwakufanya hivyo
itasaidia kuthibitisha uhalali wa tofauti ya majina na kutambulika kisheria.
Sekretarieti
ya Ajira inapenda kuwafahamisha wadau wake, hususani waombaji kazi Serikalini
kwamba haipokei barua ya utambulisho kutoka polisi inayohusu kupoteza, kuungua,
kuibiwa, utofauti wa majina kati ya cheti kimoja na kingine kutokana na baadhi
yao kuzitumia vibaya.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇