Msemaji
wa Serikali hapa nchini Assa Mwambene amekiri kutokea kwa kifo cha
Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail Nwairat kwa kujipiga risasi
mwenyewe majira ya saa saba usiku katika chumba cha ofisi za ubalozi
huo.
Mwambene alisema kuwa mpaka sasa
haijafahamika kifo cha balozi huyo kimetokana na nini, ila wafanyakazi
wa karibu katika ubalozi huo wamesema kuwa walisikia mlio wa risasi
chumbani kwake, na walipojaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa na
wakatumia nguvu ya kuvunja mlango huo na kufanikiwa kumkuta balozi yupo
katika hali ya mbaya.
Aidha walimuwahisha katika hospital ya Ami iliyopo Oysterbay na baada ya nusu saa madaktari walithibitisha kuwa amefarika dunia.
Serikali imesikitishwa na kifo
hicho na wanafanya utaratibu wote wa kuusafirisha mwili wa marehemu
kuupeleka nchini kwao kwa ajili ya mazishi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇