Rais wa TFF Jamal Malinzi |
Na EmanuelMadafa
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameandaa futari kesho (Julai 17 mwaka huu) kwa
wadau mbalimbali wa mpira wa miguu.
Shughuli
hiyo itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo waalikwa
wataanza kuwasili saa 11.30 jioni.
Waalikwa
katika futari hiyo wametoka katika makundi mbalimbali. Makundi hayo ni
wadhamini, klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza za Dar es Salaam ambazo
zitawakilishwa na watu wawili wawili.
Viongozi wa zamani wa TFF, Said El Maamry,
Leodegar Tenga, Muhidin Ndolanga, Athuman Nyamlani, Mwina Kaduguda, Michael
Wambura, Fredrick Mwakalebela na Ashery Gasabile. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
TFF waliopo Dar es Salaam, Wizara ya Michezo na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es
Salaam.
Vyama shiriki; TWFA, TAFCA, TASMA,
SPUTANZA, FRAT ambavyo vitawakilishwa na watu watatu watatu, viongozi wa Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Baraza la Michezo la Taifa
(BMT), wahariri wa habari za michezo, Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA) na Polisi kanda Maalumu- Dar es Salaam.
Wajumbe wa kamati ndogondogo za TFF
waliopo Dar es Salaam, wazee wa Simba na Yanga- watano kutoka kila klabu, timu
ya Serengeti Boys, klabu ya Saigon, Bodi ya Ligi Kuu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Wakuu wa wilaya za Dar es Salaam, wabunge wa Dar es Salaam, Meya wa Dar
es Salaam, Meya wa Kinondoni, Meya wa Ilala na Meya wa Temeke.
Waalikwa
wengine ni Omari Abdulkadir, Amin Bakhresa, Harudiki Kabunju, Hamis Kissiwa,
Ismail Aden Rage, Masoud Sanani, Jamal Bayser, Hassan Dalali, Imani Madega na
Mbaraka Igangula.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇