THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
![]() |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma
salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha mwandishi wa habari mkongwe na
mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Bwana Nkwabi
Ng’wanakilala.
Bwana
Ng’wanakilala ambaye alifariki dunia mwishoni mwa wiki kwenye Hospitali ya Rufani
ya Bugando mjini Mwanza kwa matatizo ya figo na tumbo, alizikwa jana, Jumatatu,
Julai Mosi, 2014, nyumbani kwake Kibamba, Dar es Salaam.
Katika
salamu ambazo amemtumia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Askofu Tarcisius
Ngalalekumtwa, Rais Kikwete amesema: “Kifo hiki kimelinyang’anya taifa letu mmoja
wa wanataaluma wa habari mahiri sana na mtumishi hodari wa umma ambaye
alithibitisha sifa hizo katika nafasi zote alizozishikilia. Tasnia ya habari
imepoteza kiongozi hodari.”
Ameongeza
Rais Kikwete: “Alithibitisha sifa hizo kwenye nafasi ya Ukurugenzi wa Idara ya
Habari, kwenye Ukurugenzi wa Redio Tanzania Dar Es Salaam (RTD) na kwenye
Ukurugenzi wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA). Aidha, marehemu
alithibitisha vipaji vyake siyo kwenye uandishi wa habari tu bali hata kwenye
uandishi wa vitabu, utafiti na uhadhiri, shughuli ambayo ameifanya hadi mauti
yalipomfika.”
“Naungana
na wanafamilia, wanajumuia ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustine na wanataaluma wa
tasnia yote ya habari nchini kuomboleza kifo cha Bwana Ng’wanakilala. Aidha,
naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke pema roho ya Marehemu Nkwabi
Ng’wanakilala. Amina.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR
ES SALAAM
2 Julai, 2014

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇