Mkurugenzi Mtendaji Mtendaji wa Kampuni ya Lafarge Ndugu Catherine Langreney akizungumza katika makabidhiano hayo katika eneo la mradi. |
Katibu wa ujenzi wa uwanja huo wa michezo Ndugu Solo Tuyajage akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo |
Mkuu wa Wilaya hiyo akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Lafarge namna uwanja huo utakavyo kuwa |
PICHA NA JAMIIMOJA
Na EmanuelMadafa,mbeya
Halmashauri
ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya amepokea msaada wa Tani hamsini za Cement
kutoka kiwanda cha Mbeya Cement (Lafarge) kwa lengo kupiga jeki ujenzi wa kisasa wa michezo utakaogharimu jumla ya
sh. Bilioni 8.
Aidha
uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua
watazamaji 50,000 pia unatarajiwa kuwa kitega uchumi cha aina yake kuwepo
katika wilaya ya Chunya na mkoa wa Mbeya kwa ujumla.
Akizungumza
katika makabidhiano ya msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lafarge Ndugu Catherine
Langreney amesema kuwa kampuni yake imepokea maombi hayo kutoka kwa Mkuu wa
wilaya ya Chunya na kukubali kuchangia saruji mifuko 1000 ambayo ni swan a Tani
50 .
Langreney
amesema wamepata msukumo mkubwa wa kuchangia mifuko hiyo kutokana na Halmashauri
hiyo kupanua wigo wa ajira hasa kutokana hatua yake ya kuanzisha kwa mpango wa
ujenzi wa uwanja huo.
Hata
hivyo Mkurugenzi huyo amesema kuwa msaada huo utafungua mahusiano mapya kati ya
kampuni yake na serikali ya wilaya ya Chunya katika Nyanja mbalimbali za
kimaendeleo.
Aidha
amesema kuwa mbali na kufanya biashara
kampuni yake inachangia huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi waliopo
maeneo ya karibu na kiwanda chao hivyo msaada huo ni sehemu ya huduma zao za
kawaida kwa wananchi.
Hata
hivyo Ndugu Langreney ameweka bayana kuwa kampuni yake itahakikisha inashirikiana
na Halmashauri hiyo katika ujenzi bora
wa makazi ya watu kwa kutoa teknologia mpya ya kujenga miji bora kwa hgarama
nfuu.
Akipokea msaada huo
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus
Kinawiro amesema kuwa uwanja huo unajengwa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana
na Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo pendekezo la ujenzi wa uwanja huo
aliliwasilisha kwenye vikao vya halmashauri na kuridhiwa na baraza la Madiwani.
Amesema
teyari Halmashauri ya wilaya ya Chunya
imepitisha azimio la kuchangia Sh. Milioni 70 katika bajeti yake ambapo feza
hiyo itatolewa kwa amwamu tofauti ambapo
kila mwananchi kuchangia sh.2000 kwa kwa kipindi cha miaka mitatu hadi
2016 ambapo uwanja huo utakuwa umekamilika .
Amesema
endapo uwanja huo utakamilika kwa wakati kama ilivyo pangwa uzinduzi wake
utambatana na miaka 75 ya kuanzishwa kwa Halmasahuri hiyo ambapo sherehe hizo
kufanyika ndani ya uwanja huo.
Pia
mkuu huyo wa Wilaya ametoa pongezi zake kwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo
kwa hatua yake ya kuchangia mifuko hiyo 1000 huku akiendelea kutoa wito kwa
wadau mbalimbali kuendelea kuchangia ujenzi wa uwanja huo.
Naye
Katibu wa Kamati ya Ujenzi wa uwanja huo
Solo Tuyagaje amesema kuwa hadi sasa jumla ya sh. Milioni 107 zilichangwa na
wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na makampuni yanayochimba madini wilayani humo
na wachimbaji wadogo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇