WIMBI la viongozi wa Chama kinachojiita cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kukikimbia chama hicho ziliendela leo mkoani
Tabora, kufuatia Katibu wa Chama hicho mkoani humo Othman Balozi naye kutangaza kubwaga
Manyanga na kujiunga na chama kipya cha ACT Tanzania, anaripoti Bashir Nkoromo.
Habari tulizopata kwa simu kutoka kwa wadau mkoani Tabora, zimesema kwamba, mbali na Balozi aliyewaongoza wajumbe 78
wa baraza kuu la Chadema hivi karibuni kwenda kwa msajili wa vyama kulalamikia
katiba ya Chadema kukiukwa, pia wamo viongozi mbali mbali wa mabaraza ya kimkoa
kiwilaya na majimbo walioamua kujitoa na kujiunga na Chama kipya cha
ACT-Tanzania ambacho kinaaminika kuanzishwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe (Mbunge-Chadema).
Viongozi hao ni mwenyekiti wa Bavicha
mkoa wa Tabora Hussein Kundecha,mratibu
wa uhamasishaji Bavicha wilaya ya Tabora
mjini Nzuki Machibya na Ramadhan Simba Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Bukene.
Wengine ni Suni Yohane aliyewahi kuwa katibu
wa Chadema wilaya ya Nzega pamoja na mwenyekiti wa baraza la wanawake katika
wilaya hiyo.
Wimbi hilo pia limewazoa wanachama wa
kawaida kutoka Chadema na CUF pamoja na watu 200 ambao hawakuwahi kuwa wanachama wa chama chochote hapo
awali.
Kuhama kwa viongozi hao kumekuja ikiwa
ni siku moja baada ya waliokuwa viongozi wa Chama hicho mkoa wa Kigoma kubwaga
Manyanga
Waliobwaga Manyanga kwa Mkoa wa Kigoma
hiyo juzi ni Jafari Kasisiko Mwenyekiti, katibu Msafiri Wamalwa na iti wa
Baraza la wanawake wa mkoa wa Kigoma
kubwaga Manyanga
Akizungumzia sababu ya kujiondoa Chadema
Balozi alisema kabla ya kufikia uamuzi huo alimpa taarifa mwenyekiti wake wa
mkoa Kansa Mbaruku juu ya uamuzi huo
Alisema akiwa miongoni mwa viongozi wa
awali kukipokea Chadema katika mkoa wa Tabora,amechoshwa na chama hicho kuacha
misingi yake ya kidemokrasia na
kukumbatia Ubabe na dharau huku wakiwanyooshea vidole vya usaliti wale wanaohoji baadhi ya mambo
wasiyoridhika nayo ndani ya Chama hicho.
“Leo mimi ni mtu huru na nimewasikiliza
ACT na falsafa yao ya uwazi na kuamua kujinga kwa hiari yangu sasa huu uwazi
waudhihirishe na sitasita kuhoji pale penye matatizo nawasihi katika hali hiyo
wawe wavumilivu kwa tutakayohoji”alisema Balozi.
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/697268-ccm-na-act-tanzania-wafanya-tafrija-ya-pamoja-kigoma.html
ReplyDeleteHabari hii inahusiana na hii hapo juu? Je i sahihi CCM kusherehekea wanachama kuhama CHADEMA na kuhamia ACT badala ya kuhamia CCM?