LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 8, 2014

BOMU LALIPUKA KWENYE MGAHAWA ARUSHA

IMG-20140708-WA0004
Hali ya usalama imezidi kuwa tete katika Jiji la Arusha kufuatia mfululizo wa matukio ya raia kujeruhiwa kwa kinachoaminiwa kuwa mabomu ya kurusha kwa mkono baada ya jana usiku kutokea mlipuka katika mgahawa wa Kihindi ujulikanao kama Vama Restautant uliopo maeneo ya Gymkhana.
Taarifa zinaeleza kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa huku wawili wakielezwa kuwa katika hali mbaya sana.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi wakishirikiana na Askari Jeshi wamekuwa na kazi ngumu ya kutegua kinachodhaniwa kuwa bomu kilichotegwa nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo.
Ni wakati sasa wa vyombo vya usalama kuwa imara na kazi yao. Matukio haya ni mageni mno kwa utamaduni wa Watanzania

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages