Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. George Simbachawene akiwa na wajumbe wa Bodi ya NHC na Watendaji wa NHC walipotembelea mji wa Bunggol wenye nyumba za wananchi (social housing estates) nchini Singapore kama sehemu ya ziara ya mafunzo.(Picha na Muungano Saguya-NHC)
Ujumbe wa Tanzania ukielezwa namna mji wa Singapore ulivyopangwa kulingana na matumizi mbalimbali ulipotembelea Mamlaka ya Uendelezaji Miji ya Singapore(URA) jana.
Ujumbe wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukiwa katika Bodi ya Uendelezaji wa nyumba ya Singapore ambayo harakati za Bodi hiyo zimewezesha asilimia 86 ya watu wa nchi hiyo kupata nyumba za kuishi. Nchi ya Singapore ina watu milioni 5.4
Ujumbe wa Naibu Waziri ukiwa katika kampuni inayosambaza na kusimamia usalama wa maji katika nchi ya Singapore na maeneo mbalimbali Tanzania ya Hyflux Innovation Centre ambayo pia imeonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania kusambaza maji katika maeneo inayojenga nyumba za wananchi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇