Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Naibu Mabalozi wawili.
Walioteuliwa
ni Bw. Robert Kahendaguza anayekuwa Naibu Balozi, Ubalozi
wa Kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi, na Bw.
Msafiri Marwa anayekuwa Naibu Balozi wa Tanzania London,
Uingereza.
Kabla
ya uteuzi huu, Bw. Kahendaguza alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya
Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa na Bw. Marwa alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu.
Uteuzi huu unaanza tarehe 25 Mei, 2014.
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
JUNI 11, 2014
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇