Jun 10, 2014

RAIS KIKWETE AHANI MISIBA YA KANALI MSTAAFU ALI MWANAKATWE, MCHEKESHAJI SAIDI NGAMBA "MZEE SMALL" JIJINI DAR


 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya Marehemu Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe wakati wa hafla ya kuaga mwili wa marehemu katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo, jijini Dar es Salaam  Juni 9, 2014.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba na maafisa waandamizi wa jeshi na waombolezaji  wakiwa katika shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo, jijini Dar es Salaam  Juni 9, 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwenya shughuli ya kuaga mwili wa  Marehemu Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe aliyefariki  dunia Jumamosi  asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo, jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifariji wafiwa  kwenya shughuli ya kuaga mwili wa  Marehemu Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe aliyefariki  dunia Jumamosi  asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo, jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bw. Mahmoud Saidi, Mtoto wa Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” wakati alipokwenda kuhani msiba wa msanii huyo maarufu wa filamu vichekesho nyumbani kwa  marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam Juni 9, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kuhani msiba wa msanii  maarufu wa filamu vichekesho Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa  marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam  Juni 9, 2014  Kulia ni Bw. Mahmoud Saidi, Mtoto wa Marehemu “Mzee Small”
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika dua  wakati alipokwenda kuhani msiba wa msanii  maarufu wa filamu vichekesho Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa  marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam  Juni 9, 2014 
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakifariji wafiwa   wakati walipokwenda kuhani msiba wa msanii  maarufu wa filamu vichekesho Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa  marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam Juni 9, 2014
 Mama Salma  Kikwete akimpa pole mjane wa  Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Smal”l  wakati alipokwenda kuhani msiba wa msanii huyo  maarufu wa filamu za vichekesho nyumbani kwa  marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam  Juni 9, 2014 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages