Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja huo, ambaye sasa ni Waziri wa Sheria na Katiba wa Tanzania, Dk. Asha-Rose Migiro (Mb), Walipokutana Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, jana Jumatatu.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dk. Asha-Rose kufika Umoja wa Mataifa tangu alipostaafu Unaibu Katibu Mkuu miaka miwili iliyopita.
Kabla ya Viongozi hao wawili kupiga picha hii rasmi, walikuwa na mazungumzo ya faragha.
Waziri Dk. Asha-Rose, yupo Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano ulioitishwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mchango wa Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria katika Maendeleo Endelevu baada ya 2015
Naibu Katibu Mkuu Mstaafu akipokea shada la Maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Katibu Mkuu. Ujio wa Dkt Migiro, uliamsha shamra shamra zaina yake kutoka kwa Katibu Mkuu mwenyewe ambaye kila wakati alikuwa akiachia tabasamu pana, Baraza lake la Mawaziri pamoja na wafanyakazi wa ofisi yake Binafsi pamoja na ofisi Binafsi ya Naibu Katibu Mkuu.
" Hili ua zito ngoja tukupokee" ndivyo wanayoelekea kusema Katibu Mkuu Ban Ki Moon na Mkuu wake wa Itifaki.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na timu yake akiwa ukumbini katika mazungumzo na Dk. Asha- Rose Migiro ambaye alifuatana na Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na Naibu wake, Balozi Ramadhan Mwinyi. Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu alisema, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya jambo jema kumteua Dkt. Asha-Rose Migiro kwanza kuwa mbunge na kisha kumteua kuwa Waziri anayeshughulikia Sheria na Masuala ya Katiba, akasema uzoefu wake na mchango wake siyo tu kwamba ni muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali ni muhimu pia katika Jumuiya ya Kimataifa. Ban Ki Moon alishindwa kuficha hisia zake pale aliposema mbele ya Maofisa wake kwamba siku zote amekuwa akimkumbuka Asha- Rose Migiro na kwamba amefurahi sana kwamba amepata nafasi yakufika Umoja wa Mataifa
" welcome back" ndivyo anayosema afisa huyu wakati wakisalimia kwa furana ha Naibu Katibu Mkuu Mstaafu Dk.. Asha-Rose Migiro huku Katibu Mkuu akiangalia kwa furaha
Naibu Katibu Mkuu, Bw. Jan Eliasson akimkumbatia kwa furaha Dk. Asha- Rose Migiro kabla ya kumkaribisha ofisi kwake kwa mazungumzo
Wakielekea ofisini kwa mazungumzo
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson akiwa na Dkt. Asha- Rose Migiro. Bw. Eliasson alimueleza Naibu Katibu Mkuu Mstaafu kwamba anajitahidi kufuata nyayo zake na kwamba anayo mapenzi makubwa sana na Tanzania na Afrika kwa Ujumla, Bw. Eliasson aliwahi kufanya kazi Tanzania kama mwanadiplomasi chini ya Uongozi wa Rais wa wakati huo wa Sweden Marehemu Olof Palme
Dkt. Asha- Rose Migiro akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson ( Leo Jumanne ) Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba Dkt. Asha- Rose Migiro ( Mb) atakuwa miongoni wa wanajopo ( Panellist) watakaoendesha majadiliano kuhusu mchango wa haki za binadamu na utawala wa sheria katika uungaji mkono juhudi za kitaifa na kimataifa katika kuutokomeza umaskini na maendeleo endelevu. Majadiliano hayo ni sehemu ya mkutano wa siku mbili ambao umeitishwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. John Ashe na kufunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon. Picha zote na Mpigapicha Maalum, UN
Hii ni mara ya kwanza kwa Dk. Asha-Rose kufika Umoja wa Mataifa tangu alipostaafu Unaibu Katibu Mkuu miaka miwili iliyopita.
Kabla ya Viongozi hao wawili kupiga picha hii rasmi, walikuwa na mazungumzo ya faragha.
Waziri Dk. Asha-Rose, yupo Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano ulioitishwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mchango wa Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria katika Maendeleo Endelevu baada ya 2015
Naibu Katibu Mkuu Mstaafu akipokea shada la Maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Katibu Mkuu. Ujio wa Dkt Migiro, uliamsha shamra shamra zaina yake kutoka kwa Katibu Mkuu mwenyewe ambaye kila wakati alikuwa akiachia tabasamu pana, Baraza lake la Mawaziri pamoja na wafanyakazi wa ofisi yake Binafsi pamoja na ofisi Binafsi ya Naibu Katibu Mkuu.
" Hili ua zito ngoja tukupokee" ndivyo wanayoelekea kusema Katibu Mkuu Ban Ki Moon na Mkuu wake wa Itifaki.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na timu yake akiwa ukumbini katika mazungumzo na Dk. Asha- Rose Migiro ambaye alifuatana na Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na Naibu wake, Balozi Ramadhan Mwinyi. Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu alisema, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya jambo jema kumteua Dkt. Asha-Rose Migiro kwanza kuwa mbunge na kisha kumteua kuwa Waziri anayeshughulikia Sheria na Masuala ya Katiba, akasema uzoefu wake na mchango wake siyo tu kwamba ni muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali ni muhimu pia katika Jumuiya ya Kimataifa. Ban Ki Moon alishindwa kuficha hisia zake pale aliposema mbele ya Maofisa wake kwamba siku zote amekuwa akimkumbuka Asha- Rose Migiro na kwamba amefurahi sana kwamba amepata nafasi yakufika Umoja wa Mataifa
" welcome back" ndivyo anayosema afisa huyu wakati wakisalimia kwa furana ha Naibu Katibu Mkuu Mstaafu Dk.. Asha-Rose Migiro huku Katibu Mkuu akiangalia kwa furaha
Salaam za kumlaki Dk. Asha-Rose zikiendelea kwa kila aina ya bashasha
Ban Ki Moon akiagana na Dkt. Asha-Rose Migiro baada ya mazungumzo yaoNaibu Katibu Mkuu, Bw. Jan Eliasson akimkumbatia kwa furaha Dk. Asha- Rose Migiro kabla ya kumkaribisha ofisi kwake kwa mazungumzo
Wakielekea ofisini kwa mazungumzo
Dkt. Asha- Rose Migiro akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson ( Leo Jumanne ) Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba Dkt. Asha- Rose Migiro ( Mb) atakuwa miongoni wa wanajopo ( Panellist) watakaoendesha majadiliano kuhusu mchango wa haki za binadamu na utawala wa sheria katika uungaji mkono juhudi za kitaifa na kimataifa katika kuutokomeza umaskini na maendeleo endelevu. Majadiliano hayo ni sehemu ya mkutano wa siku mbili ambao umeitishwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. John Ashe na kufunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon. Picha zote na Mpigapicha Maalum, UN
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇