Na Mwandishi Maalum, New York
Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro( Mb) amesema, ajenda za maendeleo endelevu baada ya 2015 zijielekeze zaidi katika kuyawezesha makundi ya jamii yaliyo katika mazingira magumu.
Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro( Mb) amesema, ajenda za maendeleo endelevu baada ya 2015 zijielekeze zaidi katika kuyawezesha makundi ya jamii yaliyo katika mazingira magumu.
Ameyasema hayo siku ya jumanne,wakati alipokuwa akichangia hoja kuhusu mchango wa haki za binadamu na utawala wa sheria katika kuunga mkono juhudi za kitaifa na kimataifa kuelekea upunguzaji wa umaskini na maendeleo endelevu.
Waziri Migiro alikuwa mmoja wa wanajopo wanne waliojadili hoja hiyo iliyoanzishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson ikiwa ni sehemu ya mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuwashirikisha wawakilishi kutoka mataifa mbalimbali.
Pamoja na kusisitiza haja na umuhimu wa ajenda mpya za maendeleo kujielekeza katika kuyawezesha makundi hayo ya jamii. Waziri Migiro ameongeza pia kwamba ni muhimu jumuiya ya kimataifa ikajikita pia katika kupunguza pengo la uwiano wa maendeleo kati ya maeneo ya mijini na vijijini.
“ Ni muhimu kwamba kila sehemu ya jamii ikawezeshwa ili iwe na fursa ya kupata haki, haki ya kumiliki mali, ikiwamo haki ya kumiliki na kurithi ardhi na haki za ajira zenye ujira sawa kwa kazi sawa” akaeleza Migiro na kuongeza.
Akasema ili hayo na mengineyo yaweze kutekelezwa ni vema basi suala la haki za binadamu na utawala wa sheria vikawa sehemu muhimu ya Ajenda za Maendeleo baada ya 2015 na vilevile kwa Malengo Endelevu ya Maendeleo.
Akizungumza kuhusu utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs), utekelezaji wake unaelekea ukingoni.Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba, anasema. Tangu kupitishwa kwa malengo hayo mwaka 2000 nchi nyingi hasa zile zilizokuwa zikikabiliwa na changamoto nyingi za maendeleo zilijiweka sera na vipaumbele katika utekelezaji wa malengo hayo.
“ Tumeshuhudia nguvu za pamoja katika ngazi ya kitaifa na ya kimataifa katika kuhakikisha kwamba MDGs inakuwa kiungo cha ajenda za maendeleo”. Na kuongeza kwamba pamoja na mafanikio ya kuridhisha katika utekelezaji wa MDGs hizo, bado kuna mengi yakutekelezwa”. akasisitiza Waziri.
Akizungumzi nafasi ya Tanzania katika utekelezaji wa MDGs, Waziri amesema, Tanzania imefanikiwa katika utekelezaji wa malengo mengi, ingawa changamoto kubwa imebaki katika kulitafutia ufumbuzi pengo lililopo kati ya miji na vijiji ili kuhakikisha kwamba watu wote wanakuwa na fursa na haki sawa ya kunufaika na maendeleo endelevu.
Akasema anauhakika kwamba nchi nyingi zinakabilia na changamoto hiyo ya utofauti mkubwa wa kimaendeleo kati ya maeneo ya mijini na vijijini.
“Pengo kati ya miji na vijiji ni eneo moja. lakini katika utekelezaji wa MDGS mapengo mengine hujitokeza. Ni kwa sababu hii hapana shaka kuwa haki za binadamu na utawala wa sheria ni viwezeshaji muhimu vya maendeleo” akasema.
Katika kusisitiza umuhimu wa haki za binadamu na utawala wa sheria katika kuwapatia wananchi maendeleo endelevu. Wiziri anatoa mfano kwa kusema ni jambo lisilokubalika kwamba karibu watu nne bilioni wanakosa haki zitokanazo na kutoka utawala wa sheria. Huku watoto saba kati ya kumi katika nchi zilizonyuma kimaendelo hawana vyeti vya kuzaliwa.
Waziri Migiro anaongeza kuwa “ katika nchi nyingine uwiano kati ya jaji na idadi ya watu unasimama katika jaji moja kwa watu milioni. Ili hali katika nchi nyingine, watu wanaendelea kubaguliwa kwa misingi ya makabila yao, dini au jinsia. Haya yote Mwenyekiti yanaonyesha umuhimu wa suala la haki za binadamu na utawala wa sheria kuwa sehemu ya maendeleo endelevu baada ya 2015”.
Baadhi ya washiriki wa majadiliano kuhusu mchango wa haki za binadamu na utawala bora katika kuunga mkono juhudi za kitaifa na kimataifa kuelekea upunguzaji wa umaskini na maendeleo endelevu wakimsikiliza Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba Dk. -Rose Migiro ( Mb)
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson akifungua majadiliano kuhusu mchango wa haki za binadamu na utawala wa sheria katika kuunga mkono juhudi za kitaifa na kimataifa na nafasi yake katika suala zima la maendeleo endelevu baada ya 2015. Naibu Katibu Mkuu alimtambulisha Waziri Migiro kama mtangulizi wake na katika hotuba yake alinukuu baadhi ya maneno ambayo Mhe. Migiro aliwahi kuyazungumza kuhusiana na masuala ya utawala wa sheria wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi,akifuatilia majadiliano kuhusu mchango wa haki za binadamu na utawala bora katika kusukuma mbele suala zima la upunguzaji wa umaskini na maendeleo endelevu. Wachagizaji wakuu wa majadiliano hayo alikuwa ni Mhe. Asha-Rose Migiro ( Mb) Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba, Bw. Christoph Strasser, Bw. Nicolas Lusian na Bw. Martin Kreutner.Baadhi ya washiriki wa majadiliano kuhusu mchango wa haki za binadamu na utawala bora katika kuunga mkono juhudi za kitaifa na kimataifa kuelekea upunguzaji wa umaskini na maendeleo endelevu wakimsikiliza Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba Dk. -Rose Migiro ( Mb)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇