Na Mwandishi Maalum, New York
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, jana alhamisi amezindua
rasmi mwongo wa Nishati Endelevu kwa wote (SE4ALL) wakati wa mkutano
unaohudhuriwa na wajumbe zaidi wa 1,000 wakiwamo zaidi ya mawaziri 20
wa Nishati 20 wafanyabishara, mashirika ya kimataifa yakiwamo ya
fedha na Asasi zisizokuwa za kiserikali.
Ujumbe
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu ambao ni
ulioanza Juni 4 na utamalizika Juni 6, unaongozwa na Waziri wa
Nishani na Madini Professor Sospeter Muhongo ( Mb) ambaye pamoja na
kuhudhuria na kuchangia mijadala mbalimbali, ijumaa ( June 6),
atazungumza katika mkutano wa mawaziri kuhusu nafasi ya Nishati katika
Ajenda za Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Akizindua
mwongo huo Ban ki Moon, pamoja na mambo mengine alieleza kuwa licha
ya kuwa pamoja suala la Nishati ni suala la kidunia, lakini katika
maeneo mengi ni suala linalomhusu mwanamke zaidi.
“
Ni suala linalomhusu mwanamke zaidi, linaweza kumaanisha tofauti kati
ya usalama na hofu, uhuru na utumwa , hata uhai na kifo. Dunia
lazima ije pamoja kumaliza umaskini wa nishati na kuhakikisha watu
maskini wanaweza kuhimili maisha yao na kustawi kiuchumi” akasema
Katibu Mkuu.
Akaongeza
kuwa mpango wa nishati endelevu kwa wote zimeanza kuzaa matunda na
kwamba ahadi za mabilioni ya dola zilizoahidiwa zimetolewa. Huku
nchi zinazoendelea zaidi ya 80 zimejiunga na mpango huo.
Pamoja
na Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa kuzungumza wakati wa uzinduzi wa
mwongo huo, wengine waliopata nafasi ya kuzungumza ni pamoja na Rais wa
Iceland, Olafur Ragnar Grimsson, Bw. John Ashe,Rais wa Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa na Rais wa Banki ya Dunia Jim Yong Kim ( kupitia
video) .
Mkutano
huu utafanya tathmini ya matokeo ahadi za mabilioni ya dola kuhusu
upatiakani wa nishati, ufanisi wake na nishati mbadala zilizoahidiwa
wafanyabiashara, wawekezaji na watu wengine walizotoa wakati wa Mkutano
wa Maendeleo Endelevu ( Rio+20) uliofanyika mwaka 2012.
Aidha
unatarajiwa kuhamasisha upatikanaji wa raslimali fedha, uwezeshaji
na mipango ya kufikia malengo ya nishati endelevu kwa wote.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Muhongo Sospeter Muhongo (kulia), akiwa na Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi
(kushoti), wakati wa uzinduzi wa Mwongo wa Nishati Endelevu kwa Wote.
Walioketi nyuma ni wasaizidi wa Waziri.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Mwongo wa Nishati Endelevu kwa Wote (2014-2024), uzinduzi
huo umefanyika wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka kuhusu Nishati
Endelevu kwa Wote ( SE4ALL)unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 1000. Waziri wa Nishati na
Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo ( Mb) anaongoza ujumbe wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu
Your Ad Spot
Jun 6, 2014
Home
Unlabelled
BAN KI MOON AZINDUA MWONGO WA NISHATI KWA WOTE (2014-2024 )
BAN KI MOON AZINDUA MWONGO WA NISHATI KWA WOTE (2014-2024 )
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇