Na Mwandishi Maalum, New York
Tanzania imeendelea kusisitiza kwamba, nchi ambazo hazina mpango wa kuwa na silaha za nyukilia basi ziwe na haki ya kutumia nyukilia kwa matumizi salama, na pia kupewa misaada ya kiufudi na uwezeshwaji katika eneo hilo.
Tanzania imeendelea kusisitiza kwamba, nchi ambazo hazina mpango wa kuwa na silaha za nyukilia basi ziwe na haki ya kutumia nyukilia kwa matumizi salama, na pia kupewa misaada ya kiufudi na uwezeshwaji katika eneo hilo.
Hayo yameelezwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi wakati alipokuwa akitoa maoni ya Tanzania katika mkutano wa Kamati ya Maandalizi kwaajili ya mkutano utakaofanyia tathmini utekelezaji wa Mkataba wa kuzuia usambazaji holela wa silaha za nyukilia ( NPT).
Tanzania inashiriki kikamilifu katika Mkutano huo wa maandalizi ambao ni wa wiki mbili na unafanyika Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Wanaoshiriki mkutano huu ni nchi wanachama wa NPT pamoja na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs).
Dhumuni la mkutano huu wa maandalizi, ni kuaanda dondoo na mapendekezo yatakayojadiliwa katika mkutano wa tathmini kuhusu NPT. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwakani (2015).
Akizungumza
kwa niaba ya Tanzania, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi, amesema, kama Tanzania na
kama ilivyo kwa mataifa mengi ingepeda kuona silaha za nyukilia
zinatoweka katika uso wa dunia. Lakini inaamini kwamba kila nchi
Tanzania ikiwamo inayo haki ya kuwa na fursa ya kutumia nyukilia kwa
masuala salama.
Mwakilishi huyo wa Tanzania, amebainisha kwamba, hakuna asiyetambua madhara ya silaha za nyukilia kutokana matukioa kadhaa mbayo yametokea huko nyuma yakiwamo ya Hiroshima.
Akatahadharia
kwamba kuna dalili za wazi ya kujirudia kwa madhara hayo kwa kile
alichosema Jumuiya ya kimataifa na hasa kwa nchi ambazo
zimejilimbikizia silaha hizo hazitaki konyesha nia ya kweli ya kuachana
nazo.
Akasema, inasikitisha kwamba yale mataifa ambayo yana malimbikizo ya silaha hizo, yameendelea kushikilia misimamo yao na hata kufikia mahali pa kutetea uhalali wa kuwa na silaha hizo.
Tanzania ikaeleza kwamba, silaha za nyukilia si tisho kubwa kwa nchi za Afrika, kwani tishio kubwa na ambalo linachangia katika uvunjifu wa Amani na upotevu wa maisha ya watu ni silaha ndogo ndogo na nyepesi na siyo silaha za nyukilia.
Balozi Mwinyi amewahoji washiriki wa mkutano huo, kwamba ni dunia ya aina gani tunayotaka kuwarithisha watoto wetu kwa kuendelea kukumbatia silaha hizo za maangamizi.
Akabainisha kwamba Tanzania inaamini katika Mkataba huo wa NPT kwa kile alichosema utekelezaji wake utaifanya dunia kuwa mahali salama. Na kwamba licha ya kuridhia mkataba huo, Tanzania pia ni mwanachama wa mikataba mingine ya kikanda inayohusu uthibiti wa silaha za nyukilia. Hotuba Kamili ya Balozi Mwinyi>BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇