Kaim
Mganga Mkuu Sikonge, Laurent Lushekya, akimkaribisha Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana kwenye kituo cha afya cha Kitunda kilichopo km
170 kutoka Sikonge mjini, alipofika kukagua kituo hicho cha afya leo
Mei 15, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM
na kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia ya kuzitatua
katika mkoa wa Tabora
Mganga Mfgawidhi wa Kituo cha Afya cha Kitunda, wilayani Sikonge, Dk
Sylivanus Kabatula akitoa maelezo wa Ndugu Kinana kuhusu ucheleweshwaji
wa ujenzi wa jengo la upasuaji unaofanywa na mkandarasi Humprey katika
kituo hicho cha afya, hivyo kuwakosesha wananchi huduma za matibabu
Kinana akikagua kituo cha afya Kitunda, sikonge
Kinana akikagua ofisi za Kituo hicho cha afya
Kinana akiingia kukagua jengo la maabara shule ya sekondari Kiwele, Kata ya Kitunda, Sikonge
Kinana akikagua ndani ya jengo la maabara shule ya sekondari Kiwele, Kata ya Kitunda, Sikonge
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akimsikiliza mbunge wa Sikonge Saidi Nkumba (kulia)
wakati akimweleza baadhi ya kero ambazo wapigakura wa jimbo hilo
wangependa zitatuliwe katika suala la huduma za afya. Wapili kulia ni
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mganga Mfawadhi wa Kituo
cha Afya cha Kata ya Kitunda.
Kinana akisomewa taarifa ya ujenzi wa jengo la maabara shule ya sekondari Kiwele, Kata ya Kitunda, Sikonge
Kinana akipata maelezo kuhusu ujenzi wa tanki la maji la maabara shule ya sekondari Kiwele, Kata ya Kitunda, Sikonge, leo
Kinana akikagua nyumba mpya ya mwalimu shule ya sekondari Kiwele, Kata ya Kitunda, Sikonge
Kinana akisoma vijiji vitavyopata umeme wilayani Sikonge mwaka huu wa fedha.
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia katika mkutano huo leo Mei 15, 2014,
ambapo akijibu Malalamiko ya Wananchi wa Kata ya Kitunda, alielezea
kusikishwa kwake na kitendo cha vyama vya ushirika kudaiwa kuwadhulumu
bila huruma wakulima wa tumbaku wa Kata hiyo, huku akionyesha
kushangazwa kwake na hatua ya waziri mwenye dhamana na kilimo, Chakula
na Ushirika kutotembelea wakulima kusikiliza kero zao na kuzitafutia
ufumbuzi. Mapema baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kuuliza maswali
au kutoa maoni kuhusu kero walidaikuwa zaidi y
asilimia 64 ya wakulima hawajapewa malipo yao ya mauzo ya tumbaku ya
mwaka jana na vyama vya ushirika katika Kata ya Kitunda, wilayani
Sikonge, mkoani Tabora. Pia wakulima hao walisema kuwa wanadaiwa zaidi
ya sh. bilioni 112 za mauzo hewa ya pembembejeo.
Mkulima
wa tumbaku katika Kata ya Kitunda, wilayani Sikonge, akielezea mbele ya
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana jinsi viongozi wa vyama vya
ushirika walivyosaini mkataba hewa wa pembejeo zenye thamani ya s dola
za kimarekani 150.
Mwakilishi
wa wakulima wa tumbaku katika Chama cha Ushirika cha Tumbaku Mkoa wa
Tabora ( WETCO), Lameck Mnyama, akielezea jinsi viongozi wa ushirika
huo wanavyowanyonya wakulima wa zao hilo, wakati wa mkutano wa hadhara
katika Kijiji cha Kitunda uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM ambapo
alidai hadi sasa wanaudai ushirika dola za kimarekani 76.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza kwenye mkutano huo,
ambapo aliwataka wananchi kuendelea kuiambiwa CCM matatizo na kero zao
kwa kuwa ndiyo chama chenye ridhaa yao ya kuwasimamia haki zao na siyo
vyama vingine vya siasa "Kazi
yetu CCM ni kuendelea kuisimamia Serikali ili wananchi wapate haki
zao, kwani walioomba kura kwenu ni CCM, hivyo tukikaa kimya tutalaumiwa
, najua kwa ziara hii hapa Kitunda itafanya mambo yabadilike, hiyo
ndiyo salmu yetu kwenu, asanteni" alisema Nape alipokuwa anahutubia
katika mkutano huo wa Kata ya Kitunda,
Mbunge
wa Jimbo la Sikonge, Said Nkumba akielezea kwa masikitiko jinsi
wakulima wa zao la tumbaku wanavyodhulimiwa mabilioni na viongozi wa
vyama vya ushirika wilayani Sikonge na Mkoa wa Tabora.
Wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo wa Kinana katika Kata ya Kitunda. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇