NA MWANDISHI WETU
VURUGU
na kampeni chafu zinazofanywa na baadhi ya makada wa CCM wanaojipanga
kuwania ubunge katika jimbo la Tarime, zimechukua sura mpya.
Hatua
hiyo imetokana na mbunge wa jimbo hilo Nyambari Nyangwine (pichani),
kuweka bayana kuwa atawasilisha malalamiko kwa uongozi wa CCM ngazi ya
wilaya, mkoa na taifa.
Juzi, baadhi ya wanachama wa CCM wilayani
Tarime, walilalamikia kampeni chafu zinazofanywa na baadhi makada na
kusababisha makundi ambayo ni hatari kwa Chama.
Hata hivyo,
baadhi ya makada hao ambao baadhi wametajwa kuungwa mkono na baadhi ya
viongozi wa CCM wilayani humo, wamekuwa wakieneza siasa chafu za
ukabila, jambo ambalo limeelezwa kuwa ni hatari.
Makada hao ambao
baadhi walishindwa kwenye kura za maoni, ambapo sasa wameanza kujipanga
upya lakini wakitumia njia ambazo ni kinyume na taratibu za CCM.
Taarifa
ya Nyangwine kwa vyombo vya habari jana, imesema kuwa atawasilisha
malalamiko yake ikiwa ni pamoja na kuwataja kwa majina makada hao.
Imesema kuwa makada hao wamekuwa wakieneza siasa za chuki zenye lengo la kukwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Hata
hivyo, alisema kamwe hatishwi na makada hao kwa kuwa baadhi waligombea
mara kadhaa na kushindwa hivyo jimbo hilo kutawaliwa na wapinzani kwa
miaka 10.
Alisema CCM ni chama chenye demokrasia na kinajali haki
za kila mwanachama katika kuwania uongozi, lakini kina taratibu zake
ambazo ni lazima zifuatwe ikiwa ni pamoja na kusbiri muda mwafaka wa
kufanya kampeni na si kuwahujumu waliopo madarakani.
“Nitawasilisha
malalamiko yangu rasmi kwa uongozi wa chama ngazi zote hadi kwa Katibu
Mkuu wetu (Abdulrahaman Kinana), sasa hivi ni wakati wa kutekeleza Ilani
za Chama kwa wananchi si kufanya kampeni ili kukwamisha kazi.
“Waniache
nitumikie wananchi walionichagua na muda ukifika waje tupambane kwa
hoja ndani ya Chama, haya wanayoyafanya sasa hivi ni uhuni na kutaka
kurejesha makundi ambayo mwisho wa siku yatakigharimu chama chetu.
“Baadhi
ya wanaoendesha siasa hizi chafu ni wanasiasa ambao wameishiwa sera na
goigoi na ndio sababu wameshindwa mara kadhaa kwenye uchaguzi,” alisema
Nyangwine kwenye taarifa yake.
Your Ad Spot
Apr 9, 2014
Home
Unlabelled
NYANGWINE KUWASHITAKI KWA KINANA MAKADA WANAOMHUJUMU JIMBONI
NYANGWINE KUWASHITAKI KWA KINANA MAKADA WANAOMHUJUMU JIMBONI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇