Na Mwandishi Maalum
Tanzania,
imeungana na mataifa mengine katika kusisitiza umuhimu wa nchi kumiliki mchakato
wa Mageuz iya Sekta za Usalama ( Security Sector Reform).
Akichangia majadiliano ya Baraza Kuu la
Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilikutana
kwa siku nzima ya Jumatatu wiki hii, kujadili
taarifa ya Katibu Mkuu kuhusu SSR, Naibu
Mwakilishiwa Kudumu wa Tanzania katika UN, Balozi Ramadhan Mwinyi amesema, Tanzania kama
ilivyo kwa nchi nyingine nyingi inapenda kuona kwamba mageuzi ya sekta za usalama
yanamilikiwa na nchi zenyewe zikiwamo nchi zinazotoka katika machafuko.
Katika Mkutano huo, Baraza Kuu la Usalama la
Umoja wa Mataifa, lilipitisha kwa kauli moja na kwa mara ya kwanza Azimio linalojitegemea
kuhusu mchakato wa Mageuzi ya Sektaza Usalama,kupitia azimio hilo namba 2151
(2014) pamoja na kusisitiza umuhimu wa dha
nazima ya mageuzi ya sekta za usalama na umuhimu wake kwa usalama, amani na ustawi
wa mwanadamu.
Azimio
linasisitiza kwamba umiliki wa nchi katika mageuzi hayo ni jambo la muhimu.
Akaongeza kuwa makundi ya wapiganaji na ambao
wameka silaha zao chini na kuingia katika mchakato wa majadiliano wanapaswa pia
kuwa sehemu ya mageuzi ya sekta za usalama.
Akasema kwa kuyashirikisha makundi hayo ya wapiganaji
na mengine kutasaidia ujenzi wa Amani na usalama na pia kuepusha kujirudia kwa mapigano.
Aidha Balozi Mwinyi, ameleza kwamba, nchi zinazopakana
na nchi zinazotoka kwenye machafuko pia zinayo nafasi na wajibu wa kutoa ushirikiano
na uzoefu wao katika ujenzi wa sekta za usalama.
Vile vile Balozi amebainisha kwamba katika miongo
ya miaka mitano iliyopita imedhihirisha wazi umuhimu wa jumuia za kikanda katika
uzuiaji wa mapigano, ulinziwa Amani naujenziwa Amani.
Majadiliano hayo yalifunguliwa na Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa na yaliitishwana Nigeria ambayo ni Rais wa Baraza hilo kwa Mwezi
huu wa April. Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria
Bw. Aminu Wali aliongoza majadiliano.
Wawakilishi kutoka nchi 42 wanachama waUmojawa
Mataifa, zilizungumza wakati wa majadiliano kuhusu dhana hiyo ya mageuzi ya sektaza
usalama, na bila ya kujali tofauti zao, kila moja ilisisitiza hoja ya nchi kumiliki mchakato
huo hata kwa zile ambazo zimetoka katika machafuko au mapigano.
Aidha pamoja na kusisitiza haja na umuhimu wa
nchi kumiliki mchakatohuo, zimeongeza kuwa bado kuna haja ya Jumuiya ya Kimataifa, kuziwezesha nchi hasa zile zinazotoka katika machafuko
kuweza si kujenga upya sekta hizo za usalama bali pia kuzifanyia mageuzi.
Vile vile ilisisitizwa pia kuwa mageuzi hayo ya
sekta za usalama ni muhimu katika kuziimarisha nchi ambazo ndiyo kwanza
zimetoka kwenye machafuko. Na kwamba mageuzi hayo yatapewa kipaumbele katika utekelezaji
mamlaka za ulinzi wa Amani na misheni maalum
za Kisiasa.
Wajumbe wengine walikwenda mbalizaidi, kwa kueleza
kwamba mageuzi hayo ya sektza za usalama yanapashwa kuwajumuishi kwa maana ya kushirikisha
makundi mengine ya kijamii. Lakini
kwa msisitizo kwamba serikali ndiyo iwe na mamlaka ya kuamua mfumo wa sekta zake
za usalama.
Katika salamu zake za ufunguzi Ban ki
Moon, alisema, lengo la kutekeleza mageuzi ya sekta za usalama
ambazo ni pamoja na jeshi, polisi na vyombo vya usalama ni kuwawezesha wananchi
ambao ndiyo walengwa kuishi maisha yenye usalama.
“Sektaza Usalama ndiyo muhimili mkuu wa makubaliano kati ya serikali na wananchi wake. Mamlaka ya kutumia nguvu nilazima yaendane na wajibu wa kulinda raia na kuheshimu haki za binadamu” akasemaKatibuMkuu.
Kwa mujibu wa Ban Ki Moon, sekta za usalama zinazotekeleza majukumu yake
chini ya misigi ya utawala wa sheria zina uwezo wa kuimarisha imani ya wananchi
kwa serikali yao na hivyo kuchangia katika uimara wa ujenzi wa Amani namaendeleo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇