Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza
fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza
tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na
kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani
Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na
upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga,
drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body
percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.
Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi
za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi
na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇