Uamzi huo umefanywa leo (29.4.204) katika kikao chache cha Bodi ya
Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, Bw.
Simon Sayore kutokana na kampuni hizo kukiuka masharti ya biashara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Felix Ngamlagosi, kufutwa kwa leseni hizo
kumetokana na ukikaji kwa sheria na kanuni za biashara hiyo.
Bw. Ngamlagosi katika taarifa yake,
alisema kampuni hizo zimefutiwa leseni kutokana na kukaa bila kuagiza mafuta
kama leseni inavyowataka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita tangu kupewa
leseni hizo na EWURA.
Kampuni zilizofutiwa leseni ni pamoja na
Aspam Energy (T) Limited, MPS Oil Tanzania Limited, Panone Bulk Oil Importers
Limited, Petcom (T) Limited, KMJ Tanzania Limited, Horizon Petroleum Company
Limited, G.M and Company (T) Limited na Petronas Energy Tanzania Limited.
Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeundwa chini ya sheria ya
EWURA, sura namba 414 ya Sheria za Tanzania. EWURA ina majukumu ya kusimamia
shughuli za udhibiti, kiufundi na kiuchumi
katika sekta Nne (4) za Petroli, Umeme, Gasi Asili na Maji Safi na
Maji Taka.
IMETOLEWA NA
BW. FELIX
NGAMLAGOSI
MKURUGENZI
MKUU
EWURA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇