Mkurugenzi Mkuu, Idara Kuu ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa
anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 45 wa Kamisheni ya
Takwimu ya Umoja wa Mataifa, akifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi
wa mkutano huo wa wiki moja Unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya nchi 24 ambazo ni
Wajumbe wa Kamisheni hiyo. Mkutano wa Kamisheni ulifunguliwa na Bw.
WU HONGBO, Katibu Mkuu Msaidizi anayeongoza Baraza la Umoja wa Mataifa
la Uchumi na Maendeleo ya Jamii ( ECOSOC) Katika Hotuba yake Bw.
HONGBO ametoa changamoto kwa wataalamu hao wa Takwimu ya kuhakikisha
kwamba wanafuatilia kwa karibu majadiliano yanayoendelea kuhusu ajenda
mpya za maendeleo endelevu baada ya 2015 kwa kile alichosema,
utekelezaji wa malengo hayo utahitaji kuungwa mkono na takwimu rasmi na
endelevu.
Na Mwandishi Maalum, New Yok
Wajumbe
wanaohudhuria Mkutano wa 45 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa
Mataifa, wamepewa changamoto ya kuhakikisha kwamba, Takwimu rasmi na
sahihi zinaunga mkono pamoja na mambo mengine, utekelezaji na
usimamizi wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) baada ya 2015.
Changamoto
hiyo imetolewa siku ya Jumanne na Katibu Mkuu Msaidizi Bw. WU HONGBO
anayeongoza Baraza la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya Uchumi
na Maendeleo ya Jamii ( ECOSOC). Bw. HONGBO alikuwa akifungua rasmi
mkutano wa wiki moja wa wajumbe wanaounda Kamisheni ya Takwimu ya Umoja
wa Mataifa.
Wajumbe
hao ni kutoka nchi 24 ikiwamo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo
ujumbe wake katika Mkutano huu unaongozwa na Dkt. Albina Chuwa,
Mkurugenzi Mkuu wa Idara Kuu ya Taifa ya Takwimu.
Bw.
WU HONGBO amewaeleza wataalamu hao wa masuala ya Takwimu kwamba,
mwezi wa Tisa mwaka huu, Umoja wa Mataifa, utaandaa mikutano kadhaa ya
kilele, ukiwamo Mkutano wa Tatu wa Kimataifa kuhusu maendeleo ya
mataifa ya visiwa vidogo.
Ni
katika kipindi hicho hicho pia ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
amewaalika Wakuu wa Nchi na Serikali, wafanyabiashara, vyama visivyo
ya kiserikali, na watu wa kada mbalimbali kuhudhuria mkutano wa kilele
kuhusua masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi.
“
Hivi sasa kuna mchakato unaoendelea wa majadiliano ya wazi ya
Kikundi Kazi kuhusu ajenda mpya za Malengo ya Maendeleo Endelevu baada
ya 2015 ( SDGs).
Majadiliano
haya na mengine , ni wazi kwamba nafasi na mchango wa Takwimu ni
muhimu sana katika kuchangia na kutoa mwongozo wa uundaji wa será na
uundwaji wa kamati za ufuatiliaji wa utekeleazaji wa makubaliano
yatakayofikiwa” akasisitiza Katibu Mkuu Msaidizi.
Katika kuhakikisha
kwamba, wataalamu hao kutoka Taasisi za Kitaifa za Takwimu
wanafuatilia kwa karibu mikutano mbalimbali muhimu inayoendelea
katika Umoja wa Mataifa, yakiwamo majadiliano ya Kikosi Kazi kuhusu
Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Katibu
Mkuu Msaidizi, Bw. HONGBO amesema, wakati mkutano huo wa Kamishieni ya
Takwimu ukifanyika, katika ukumbi mwingine, kulikuwa kukiendelea
majadiliano ya awamu ya tisa kuhusu maendeleo endelevu baada ya 2015.
“
Wiki hii inatoa fursa ya aina yake kwenu, pamoja na ajenda mbalimbali
zinazowakutanisha hapa, na wakati huu mkiendelea na mkutano wenu,
kuna mkutano unaoendelea kuhusu maandalizi ya malengo mapya ya
maendeleo.
Itakuwa
vema na ni matumaini yangu kuwa mtaitumia fursa hii kuwasiliana na
kubadilishana mawazo na wajumbe wenzenu wanaohudhuria mkutano huo.
Lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba malengo hayo mapya ya maendeleo
endelevu utekelezaji wake unaungwa mkono na Takwimu rasmi na endelevu”
akasisitiza.
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ni kati ya nchi 30 ambazo ziliteuliwa kushiriki
katika majadiliano ya Kikosi Kazi kuhusu maandalizi hayo ya SGDs
baada ya 2015.
Katika
mzunguko huu wa tisa wa majadiliano wa hayo kuhusu SDGs, Tanzania
inawakilishwa na Dkt. Lorah Madete, Afisa Mkuu na mchambuzi wa Sera
kutoka Ofisi ya Rais, Kamisheni ya Mipango.
Your Ad Spot
Mar 5, 2014
Home
Unlabelled
TAKWIMU RASMI NA ENDELEVU NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA SERA ZA MAENDELEO -UMOJA WA MATAIFA
TAKWIMU RASMI NA ENDELEVU NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA SERA ZA MAENDELEO -UMOJA WA MATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇