Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na kinamama wa hamasa, baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika, Jumapili, Machi 30, 2014, katika mji mdogo wa Namanyere, wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kizitatua, katika mkoa wa Rukwa.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano huo uliofanyika katika mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Jumapili, Machi 30, 2014.
Kijana Elias Yeremia akimuuliza swali Kinana jukwaani, katika mkutano huo wa Namanyere, Nkasi mkoani Rukwa
Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume akihutubia mkutano huo wa Namanyere
Vijana wa Namanyere wakiwa wamepanda juu ya lori siyo kwa lengo la kusafiri bali kuhakikisha wanamuona Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere
Wazee wakimsikiliza kwa makini Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere
Mamia ya wananchi kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete, akimshukuru Kinana kwa hotuba nzuri, mkuatno huo wa Namanyere
Kikundi cha matarumbeta kikitoa burudani kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
Mzee Rogas Nkana akimpatia ushahidi wa vielelezo na nyaraka mbalimbali kuhusu mirathi ya binti yake ambayo amefuatilia kwa muda mrefu hadi sasa bila mafanikio. Mzee Nkana alidai mbele ya Kinana kwamba madai hayo kwa ajili ya mirathi ya kifo cha binti yake ambaye alifariki dunia mwaka 2000 akiwa mtumishi wa Wirzara ya Mambo ya Ndani katika Jeshi la Uhamiaji yamekuwa kitendawili licha ya kufuatilia katika ofisi husika. Mzee Nkana alipata fursa hiyo wakati Kinana alipoamua kukutana na waasisi wa Chama na mabalozi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali katika ukumbi wa Community Centre katika mji mdogo wa Namayere wilayani Nkasi. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog
Your Ad Spot
Mar 31, 2014
Home
Unlabelled
KINANA NDANI YA MJI MDOGO WA NAMANYERE, WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA
KINANA NDANI YA MJI MDOGO WA NAMANYERE, WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇