CHAMA
Cha Mapinduzi (CCMI mkoani Shinyanga kimepata pigo baada ya kuondokewa
na mmoja wa makada wake maarufu ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa CCM
katika kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga, Paul Zephania (61)
aliyefariki dunia jana baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga,
Khamis Mgeja kifo cha kada huyo kimeacha pengo kubwa kwa wana CCM wa
wilaya ya Shinyanga na mkoa kwa ujumla kutokana na juhudi zake za
uimarishaji wa chama alizokuwa akizifanya wakati wa uhai wake.
Mgeja
alisema Zephania ameacha pengo kubwa kwa CCM ambalo litachukua mda
kuzibika kutokana na shughuli alizokuwa akizifanya ndani ya chama, na
kudai kuwa marehemu alikuwa mkalimu, mpole mwenyekujishusha,kujituma na
alikuwa tiyali kuachashughuli zake binafsi kwa ajili ya kukitumikia
Chama
Akiongoza
mazishi ya kada huyo kijijini kwake Iselamagazi jana, Mgeja alisema
marehemu Zephania alijiunga na chama cha mapinduzi tangu mwaka 1978 na
mwaka 2002 alikuwa katibu wa tawi CCM wilayani humo, na mnamo mwaka
2012 alikuwa mwenyekiti wa kata ya Iselamagazi hadi mauti kumfika
“Kwa kweli
CCM tumepata pigo kubwa kwa kuondokewa na kiongozi wetu shupavu ambaye
amekitumikia Chama kwa mda mrefu sana (36),tangu ajiunge na CCM alikuwa
mchapa kazi na haja wahi kulalamikiwa na mtu yeyote na ndio maana mnaona
maelfu ya watu Mmekuja kumpumzisha kwenye makazi yake ya milele kwa
sababu alikuwa mtu wa watu’’ alisema mgeja
Mgeja
pia alitoa pole katika familia ya marehemu pamoja na wakazi wa kata
hiyo ya Iselamagazi kuwa chama cha mapinduzi CCM kipopamoja nao katika
kuomboleza kifo cha mpendwa wao na kuwa ambia kuwa wasihuzunike sana
kwani mwenyezi mungu kampenda zaidi
Katika
hatua nyingine mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni
mjumbe wa NEC alitumia fursa hiyo kuwaeleza viongozi mbalimbali wa madehemu ya dini waliohudhulia
mazishi hayo kwamba CCM inatambua mchango wao katika kuielimisha jamii
na kuwaomba waendelee kutoa elimu kwa jamii kupitia mahubiri yao ya kila
siku na kuliombe taifa liendelee kuwa na amani.
Kwa
upande wake msemaji wa familia Emiliani Lucas akisoma historia ya
marehemu enzi za uhai wake alisema alizaliwa mwaka 1953 katika kijiji
cha Mwang’oye wilayani humo, na kwamba marehemu aliugua ugonjwa wa
malaria mnamo Machi 14 mwaka huu na kufariki Machi 18 saa 12 jioni.
Marehemu
ameacha mjane mmoja, watoto kumi na moja, na wajukuu 21, mazishi hayo
pia yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na seriikali mkoani
Shinyanga wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM wa mkoa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇