Kamati Ndogo ya Maadili ya
CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip
Mangula leo imewahoji watu watatu ambao wawili walishawahi kuwa
Mawaziri Wakuu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Mawaziri hao waliohojiwa leno ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward
Lowasa,Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye na Mbunge wa
Sengerema Ndugu William Ngeleja ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa
Nishati na Madini.
Kamati hiyo bado ina kazi ya kuwahoji viongozi wengine watatu ambao leo walishindwa kufika baada ya kuomba hudhuru kwani walikuwa na majukumu mengine ya kiserikali, ambao hawajafika leo ni Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Bernard Membe ambaye yupo safarini nje ya nchi ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen Wassirana Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu Januari Makamba.

Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye akiwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma tayari kwa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili.
Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa akizungumza na Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye kabla ya kuanza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma.
Ndugu William Ngeleja akisubiri kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama.
Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa kizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi.
Waandishi wa Habari wakiwajibika kuandika habari nje ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo viongozi watatu walihojiwa na Kamati ndogo ya Maadili.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇