THE UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA RASMI
KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA
KATIBA
UTANGULIZI
1.
Uteuzi wa
Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura,
83 (The Constitutional Review Act, Cap
83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na
mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la
Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha
umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.
2.
Sheria hii
inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama
ifuatavyo:-
(i)
Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii)
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii)
Wajumbe 201 kwa
mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.
3.
Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-
(i)
Taasisi
zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii)
Taasisi za
Kidini (20)
(iii)
Vyama vyote
vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv)
Taasisi za
Elimu (20);
(v)
Watu wenye
Ulemavu (20);
(vi)
Vyama vya
Wafanyakazi (19);
(vii)
Vyama
vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii)
Vyama vinavyowakilisha
wavuvi (10);
(ix)
Vyama vya
Wakulima (20); na
(x)
Vikundi vya
Watu wenye Malengo yanayofanana (20).
4.
Mchakato wa
uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13
Desemba, 2013. Tangazo hilo
lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa
kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum
la Katiba. Aidha, Tangazo hilo
la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini.
Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi
na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe
02/01/2014.
5.
Mapendekezo
hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar,
mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
6.
Kufuatia
mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha
mapendekezo yao .
Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762
kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo basi, taasisi na makundi
mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636.
Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118
walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.
7.
Mchanganuo wa
idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama
ifuatavyo:
|
Kundi/Taasisi
|
Taasisi
zilizoleta mapendekezo
|
Idadi
ya Watu Waliopendekezwa
|
Wanaota-kiwa
|
Idadi ya Walioteuliwa
|
|||
Tz
Bara
|
Z’bar
|
Tz
Bara
|
Z’bar
|
Tz
Bara
|
Z’bar
|
|||
1.
|
Taasisi zisizokuwa
za Kiserikali
|
246
|
98
|
1,203
|
444
|
20
|
13
|
7
|
2.
|
Taasisi za Kidini
|
55
|
17
|
344
|
85
|
20
|
13
|
7
|
3.
|
Vyama vya Siasa
vyenye Usajili wa Kudumu
|
21
|
14
|
129
|
69
|
42
|
28
|
14
|
4.
|
Taasisi za Elimu
|
9
|
9
|
84
|
46
|
20
|
13
|
7
|
5.
|
Makundi ya Walemavu
|
24
|
6
|
97
|
43
|
20
|
13
|
7
|
6.
|
Vyama vya
Wafanyakazi
|
20
|
1
|
89
|
13
|
19
|
13
|
6
|
7.
|
Vyama
Vinavyowakilisha Wafugaji
|
8
|
1
|
43
|
4
|
10
|
7
|
3
|
8.
|
Vyama vinavyowakilisha
Wavuvi
|
7
|
3
|
45
|
12
|
10
|
7
|
3
|
9.
|
Vyama vya Wakulima
|
22
|
8
|
115
|
44
|
20
|
13
|
7
|
10.
|
Makundi yenye
Malengo Yanayofanana
|
142
|
21
|
613
|
114
|
20
|
14
|
6
|
|
Mapendekezo Binafsi
|
-
|
-
|
118
|
-
|
|
|
|
|
Jumla
|
672
|
178
|
2,880
|
874
|
201
|
134
|
67
|
|
Jumla Kuu
|
850
|
3,754
|
|
|
|
8.
Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba.
Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar
na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe
201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar
na wajumbe 134 watatoka Tanzania
Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe
hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya
siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata
wajumbe 201 halikuwa rahisi hata
kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
9.
Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka
Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati
nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande
wa Zanzibar ,
majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874
ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67
wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni
kwamba ukichukua taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara
walipendekezwa watu 1,203, wakati
nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13
tu. Kwa upande Zanzibar ,
taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444
ikilinganishwa na nafasi 7 tu
zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.
WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
10.
Rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
wakishirikiana na Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe
walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
(a)
Uteuzi
umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana, watu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana
yaani wenye umri wa kati miaka 22-35,
ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa
kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri
wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b)
Sheria inataka
kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa
ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa
vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.
(c)
Uwakilishi wa
vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na
wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa
kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili
wameteuliwa kutoka katika kila chama.
Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo
ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge
Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:
TAASISI ZISIZOKUWA ZA
KISERIKALI- (WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Magdalena Rwebangira
|
2.
Kingunge Ngombale Mwiru
|
3.
Asha D. Mtwangi
|
4.
Maria Sarungi Tsehai
|
5.
Paul Kimiti
|
6.
Valerie N. Msoka
|
7.
Fortunate Moses Kabeja
|
8.
Sixtus Raphael Mapunda
|
9.
Elizabeth Maro Minde
|
10.
Happiness Samson Sengi
|
11.
Evod Herman Mmanda
|
12.
Godfrey Simbeye
|
13.
Mary Paul Daffa
|
|
|
|
1.
Idrissa Kitwana Mustafa
|
2.
Siti Abbas Ali
|
3.
Abdalla Abass Omar
|
4.
Salama Aboud Talib
|
5.
Juma Bakari Alawi
|
6.
Salma Hamoud Said
|
7.
Adila Hilali Vuai
|
|
|
|
TAASISI
ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Tamrina Manzi
|
2.
Olive Damian Luwena
|
3.
Shamim Khan
|
4.
Mchg. Ernest Kadiva
|
5.
Sheikh Hamid Masoud Jongo
|
6.
Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo
Mtetemela
|
7.
|
8.
Hamisi Ally Togwa
|
9.
Askofu Amos J. Muhagachi
|
10.
Easter Msambazi
|
11. Mussa
Yusuf Kundecha
|
12.
Respa Adam Miguma
|
13. Prof.
Costa Ricky Mahalu
|
|
|
|
1.
Sheikh Thabit Nouman Jongo
|
2.
Suzana Peter Kunambi
|
3.
Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu
|
4.
Fatma Mohammed Hassan
|
5.
Louis Majaliwa
|
6.
Yasmin Yusufali E. H alloo
|
7.
Thuwein Issa Thuwein
|
|
|
|
VYAMA VYOTE VYA SIASA
VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE
42)
|
|
|
|
1.
Hashim Rungwe Spunda
|
2.
Thomas Magnus Mgoli
|
3.
Rashid Hashim Mtuta
|
4.
Shamsa Mwangunga
|
5.
Yusuf S. Manyanga
|
6.
Christopher Mtikila
|
7.
Bertha Ng’angompata
|
8.
Suzan Marwa
|
9.
Dominick Abraham Lyamchai
|
10.
Mbwana Salum Kibanda
|
11.
Peter Kuga Mziray
|
12.
Isaac Manjoba Cheyo
|
13.
Dr. Emmanuel John Makaidi
|
14.
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
|
15.
Modesta Kizito Ponera
|
16.
Prof. Abdallah Safari
|
17.
Salumu Seleman Ally
|
18.
James Kabalo Mapalala
|
19.
Mary Oswald Mpangala
|
20.
Mwaka Lameck Mgimwa
|
21.
Nancy S. Mrikaria
|
22.
Nakazael Lukio Tenga
|
23.
Fahmi Nasoro Dovutwa
|
24.
Costantine Benjamini Akitanda
|
25.
Mary Moses Daudi
|
26.
|
27.
John Dustan Lifa Chipaka
|
28.
Rashid Mohamed Ligania Rai
|
|
|
1.
Ally Omar Juma
|
2.
Vuai Ali Vuai
|
3.
Mwanaidi Othman Twahir
|
4.
Jamila Abeid Saleh
|
5.
Mwanamrisho Juma Ahmed
|
6.
Juma Hamis Faki
|
7.
Tatu Mabrouk Haji
|
8.
Fat –Hiya Zahran Salum
|
9.
Hussein Juma
|
10.
Zeudi Mvano Abdullahi
|
11.
Juma Ally Khatibu
|
12.
Haji Ambar Khamis
|
13.
Khadija Abdallah Ahmed
|
14.
Rashid Yussuf Mchenga
|
TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Dr. Suzan Kolimba
|
2.
Prof. Esther Daniel Mwaikambo
|
3.
Dr. Natujwa Mvungi
|
4.
Prof. Romuald Haule
|
5.
Dr. Domitila A.R. Bashemera
|
6.
Dr. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa
|
7.
Prof. Bernadeta Kilian
|
8.
Teddy Ladislaus Patrick
|
9.
Dr. Francis Michael
|
10.
Prof. Remmy J. Assey
|
11.
Dr. Tulia Ackson
|
12.
Dr. Ave Maria Emilius Semakafu
|
13.
Hamza Mustafa Njozi
|
|
TANZANIA ZANZIBAR (7)
|
|
1.
Makame Omar Makame
|
2.
Fatma Hamid Saleh
|
3.
Dr. Aley Soud Nassor
|
4.
Layla Ali Salum
|
5.
Dkt. Mwinyi Talib Haji
|
6.
Zeyana Mohamed Haji
|
7.
Ali Ahmed Uki
|
|
|
|
WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Zuhura Musa Lusonge
|
2.
Frederick Msigala
|
3.
Amon Anastaz Mpanju
|
4.
Bure Zahran
|
5.
Edith Aron Dosha
|
6.
Vincent Venance Mzena
|
7.
Shida Salum Mohamed
|
8.
Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi.
|
9.
Elias Msiba Masamaki
|
10.
Faustina Jonathan Urassa
|
11.
Doroth Stephano Malelela
|
12.
John Josephat Ndumbaro
|
13.
Ernest Njama Kimaya
|
|
|
|
1.
Haidar Hashim Madeweyya
|
2.
Alli Omar Makame
|
3.
Adil Mohammed Ali
|
4.
Mwandawa Khamis Mohammed
|
5.
Salim Abdalla Salim
|
6.
Salma Haji Saadat
|
7.
Mwantatu Mbarak Khamis
|
|
VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)
|
|
|
|
1.
Honorata Chitanda
|
2.
Dr. Angelika Semike
|
3.
Ezekiah Tom Oluoch
|
4.
Adelgunda Michael Mgaya
|
5.
Dotto M. Biteko
|
6.
Mary Gaspar Makondo
|
7.
Halfani Shabani Muhogo
|
8.
Yusufu Omari Singo
|
9.
Joyce Mwasha
|
10.
Amina Mweta
|
11.
Mbaraka Hussein Igangula
|
12.
Aina Shadrack Massawe
|
13.
Lucas Charles Malunde
|
|
|
|
1.
Khamis Mwinyi Mohamed
|
2.
Jina Hassan Silima
|
3.
Makame Launi Makame
|
4.
Asmahany Juma Ali
|
5.
Mwatoum Khamis Othman
|
6.
Rihi Haji Ali
|
|
|
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE
10)
|
|
|
|
1.
William Tate Olenasha
|
2.
Makeresia Pawa
|
3.
Mabagda Gesura Mwataghu
|
4.
Doreen Maro
|
5.
Magret Nyaga
|
6.
Hamis Mnondwa
|
7.
Ester Milimba Juma
|
|
|
|
1.
Said Abdalla Bakari
|
2.
Mashavu Yahya
|
3.
Zubeir Sufiani Mkanga
|
|
|
|
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI
–(WAJUMBE 10)
|
|
|
|
1.
Hawa A. Mchafu
|
2.
Rebecca Masato
|
3.
Thomas Juma Minyaro
|
4.
Timtoza Bagambise
|
5.
Tedy Malulu
|
6.
Rebecca Bugingo
|
7.
Omary S. Husseni
|
|
|
|
1.
Waziri Rajab
|
2.
Issa Ameir Suleiman
|
3.
Mohamed Abdallah Ahmed
|
|
VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Agatha Harun Senyagwa
|
2.
Veronica Sophu
|
3.
Shaban Suleman Muyombo
|
4.
Catherine Gabriel Sisuti
|
5.
Hamisi Hassani Dambaya
|
6.
Suzy Samson Laizer
|
7.
Dr. Maselle Zingura Maziku
|
8.
Abdallah Mashausi
|
9.
Hadijah Milawo Kondo
|
10.
Rehema Madusa
|
11.
Reuben R. Matango
|
12.
Happy Suma
|
13.
Zainab Bakari Dihenga
|
|
|
|
1.
Saleh Moh’d Saleh
|
2.
Biubwa Yahya Othman
|
3.
Khamis Mohammed Salum
|
4.
Khadija Nassor Abdi
|
5.
Fatma Haji Khamis
|
6.
Asha Makungu Othman
|
7.
Asya Filfil Thani
|
|
|
|
WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA –
(WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Dr. Christina Mnzava
|
2.
Paulo Christian Makonda
|
3.
Jesca Msambatavangu
|
4.
Julius Mtatiro
|
5.
Katherin Saruni
|
6.
Abdallah Majura Bulembo
|
7.
Hemedi Abdallah Panzi
|
8.
Dr. Zainab Amir Gama
|
9.
Hassan Mohamed Wakasuvi
|
10.
Paulynus Raymond Mtendah
|
11.
Almasi Athuman Maige
|
12.
Pamela Simon Massay
|
13.
Kajubi Diocres Mukajangwa
|
14.
Kadari Singo
|
|
|
1.
Yussuf Omar Chunda
|
2.
Fatma Mussa Juma
|
3.
Prof. Abdul Sheriff
|
4.
Amina Abdulkadir Ali
|
5.
Shaka Hamdu Shaka
|
6.
Rehema Said Shamte
|
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es
Salaam.
7 Februari, 2014
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇