Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akifanya mahojiano na Mwandishi wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) Erick David Nampesya leo Jijini Dar es Salaam. |
(Picha na Hassan Silayo)
Frank Mvungi
Serikali ya Tanzania
imesema haina ugomvi na nchi jirani kwa
kuwa ni wadau wa maendeleo katika kujenga uchumi imara kwa kutumia fursa zilizopo.
Hayo yamesemwa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe wakati
akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam kuhusu taarifa
mbalimbali zinazoripotiwa na vyombo vya habari kuhusu uhusiano wa Tanzania na
Rwanda.
Akieleza zaidi Mh.Membe
alisema vyombo vya habari vinalojukumu
kubwa la kuielimisha jamii na kuimarisha uhusiano kati Tanzania na nchi jirani
na si kufanya jambo lolote linaloweza kuleta tofauti kati ya Taifa moja na
jingine.
Mh. Membe amesema kuwa Tanzania
ni nchi inayotumia njia za Kidiplomasia kuondoa tofauti zozote zitakazojitokeza
kati yake na nchi yoyote na haina mpango
wa kuingia kwenye mgogoro na nchi yoyote ile.
Aliongeza kuwa Tanzania
kwa miaka mingi imekuwa kisiwa cha amani na mfano bora katika bara la Afrika
ndio maana imekuwa mstari wa mbele katika kutatua migogoro ndani ya bara la
Afrika.
Akifafanua zaidi Mh.
Membe amesema Tanzania imepeleka vikosi vyake
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Lebanon,Sudan ya Kusini, katika kutimiza
jukumu la kulinda amani Duniani.
“Tunafikri ni vyema
Jukumu la ulinzi wa Bara la Afrika
likawa mikononi mwa Afrika yenyewe” alisisitiza Mh.Membe alipokuwa akifafanua
kuhusu nafasi ya Tanzania katika kuleta amani katika mataifa mbalimbali ndani
na nje ya Bara la Afrika.
Pia alieleza kuwa tangu
harakati za ukombozi wa bara la Afrika Tanzania imekuwa makao makuu ya vyama vyote vya ukombozi
barani Afrika na kusaidia katika harakati za kuleta ukombozi .
Serikali ya Tanzania
kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mwaka huu imepanga
kufanya maandalizi mazuri yatakayoiwezesha timu ya Taifa kushiriki na kupata
medani katika michezo ya jumuiya ya madola.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇