Na Mwandishi Maalum, NEW YORK
Wakati Serikali ya Tanzania ikijipanga kwa utekelezaji wa awamu ya pili ya Operesheni Tokomeza Ujangili, Bunge la New York, nchini Marekani, kupitia Kamati yake ya Hifadhi ya Mazingira linajipanga kuangalia namna ya kuboresha ufanisi wa sheria na kanuni zinazolinda na kudhibiti biashara ya pembe za Tembo na wanyama wengine.
Wakati Serikali ya Tanzania ikijipanga kwa utekelezaji wa awamu ya pili ya Operesheni Tokomeza Ujangili, Bunge la New York, nchini Marekani, kupitia Kamati yake ya Hifadhi ya Mazingira linajipanga kuangalia namna ya kuboresha ufanisi wa sheria na kanuni zinazolinda na kudhibiti biashara ya pembe za Tembo na wanyama wengine.
Katika kutekeleza azima hiyo, jana alhamisi, hapa New York, Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi ya Mazingira Robert K. Sweeney (Mb) aliitisha mkutano public hearing) uliokuwa na lengo la kusikiliza michango na maoni kutoka kwa wadau mbalimbali, michango ambayo kwa namna moja ama nyingine itachangia katika uboreshaji wa sheria na sera zilizopo hivi sasa.
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, alikuwa miongoni mwa waalikwa waliopewa fursa ya siyo tu, kutoa ushuhuda wa ukubwa wa tatizo la ujangili na adhari zake. Lakini pia kuelezea nini mamlaka husika zinafanya kukabiliana na tatizo hilo na kutoa ushauri na mapendekezo ya hatua zaidi za kukabiliana na changamoto hiyo.
Pamoja na kuwasilisha ushuhuda wake na hatua zinazochuliwa na serikali, Balozi Manongi pia alijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na Mwenyekiti wa Kamati na wajumbe wengine.
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi ya Mazingira, Robert Sweeney alisema. Tembo wa Afrika ambao ni urithi wa dunia na muhimu kwa ustawi wa mwanadamu wamo hatarini kutoweka kama hatua madhubuti zaidi hazitachukuliwa.
Akatahadharisha kuwa uwindaji haramu wa tembo kwaajili ya pembe zao siyo tu kwamba umekidhiri na kuongezeka badala ya kupungua, lakini pia hivi sasa mitandao ya mbalimbali ya uhalifu na ugaidi inajiingiza kwa kasi katika eneo hilo.
“Hali ni mbaya, mauaji ya tembo yanaongezeka, tunahitaji kuchukua hatua zaidi na ndio maana nimeitisha mkutano huu ili kuangalianamna gani sheria na kanuni zetu zilizopo zitaweza kuwa na ufanisi zaidi katika kudhibiti biashara ya meno ya tembo” akasema Mwenyekiti.
Akabinisha kwamba katika New York biashara ya meno ya tembo inadhibitiwa kupitia sheria na kanuni mbalimbali lakini pamoja na sheria hizo, bado New York inaongoza katika Marekani kwa kuwa kituo cha biashara ya pembe za tembo.
Akatoa mfano kwa kueleza kuwa katika mwaka 2012, pembe za tembo zenye dhamani ya dola 2 milioni ambazo ziliingia New Yor kwa njia zisizo halali zilikamatwa na kutekezwa. Na kwamba tatizoni kubwa.
Akitoa ushuhuda wake, Mwakilishi wa Tanzania Balozi Manongi, alielezea kwa kina namna ambavyo Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete inavyoshughulia tatizo la ujangili na biashara haramu ya pembe za tembo.
Akasema utekelezaji wa sheria, será na kanuni mbalimbali unachangamoto nyingi lakini Serikali haijakata tamaa imejipanga vyema ili kuhakikisha kwamba uridhi huo wa Tanzania na dunia kwa ujumla haupotei kabisa.
Akasema tisho la kutoweka kwa tembo si la nadharia ni la kweli kabisa na kwa sababu hiyo akasema Tanzania inaunga mkono juhudi za kimataifa za kukabiliana na ujangili na itakuwa tayari kushirikiana na wadau mbalimbali kuokoa Tembo wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Akarudia wito ambao umekuwa ukitolewa mara kwa mara na Mhe. Rais Kikwete kwamba, njia mojawapo na muhimu ya kukabiliana na biashara ya pembe za tembo ni kudhibiti soko la bidhaa hiyo.
Hata hivyo akasema, umaskini pia unachangia kwa baadhi ya watu kujihusisha na kushirikiana na majangili kama njia ya kujipatia kipato. Kusoma zaidi alichosema Balozi Manongi>BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇