LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 25, 2013

MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA CCM MJINI DODOMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Mweneyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipowasili Makao Makuu ya CCM, Jengo la White House, mjini Dodoma, kufunga mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa, jana, Oktoba 24, Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula.
 Mweneyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akionyesha kuwa mwenye furaha, alipowasili ukumbini kufunga mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa, jana, Oktoba 24, 2013 mjini Dodoma. Mafunzo hayo yaliyokuwa ya siku nne yalifunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Ukumbi ukilipuka kwa mbinje, nderemo na vifijo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipowasili ukumbini, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma kufunga mafunzo ya watendaji na viongozi wa CCM.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, baada ya kuwasilini ukumbini na kulakiwa kwa shangwe na wahitimu wa mafunzo kwa wa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya nchini mjini Dodoma, jana, Oktoba 24, 2013.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya watendaji na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa hapa nchini, mjini Dodoma , jana , Oktoba 25, 2013. Kushoto ni Kinana na Kulia ni Mangula.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akizungumza namna mafunzo hayo yalivyoandaliwa na Idara yake ya Itikadi na Uenezi na kumalizika kwa mafanikio makubwa.
 Baadhi ya viongozi wa Jumuia na Sekretarieti wakiwa ukumbini
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akitazama bango jipya la picha za wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, baada ya mabango hayo kugawiwa kwa washiriki wa mafunzo hayo ukumbini, wakati wa kufungwa mafunzo hayo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
 Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye akihamasisha baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kifunga mafunzo hayo.
 VYETI TUTAGAWA KAMA HIVI: Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisema hivyo huku akimshika mkono mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Bashir Nkoromo, kabla ya kuanza kugawa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM, ngazi za wilaya na mikoa, jana Oktoba 24, 2013, mjini Dodoma. Nkoromo ambaye ni Mpigapicha Mwandamizi wa Uhuru Publications Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Uhuru,Mzalendo na Burudani,  ni Katibu Msaidizi katika Kitengo cha Mawasiliano na Umma, Idara ya Itikadi na Uenezi, CCM, Taifa.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Makatibu wa CCM wa mikoa, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi, alipofunga mafunzo ya utendaji bora kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa., jana, Oktoba, 24, Makao Makuu ya CCM mjini Dopdoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Watatu ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdultahman Kinana. Zaidi ya makatibu wa CCM wa mkoa wa wilaya zote nchini wamehitimu mafunzo hayo. Imetayarishwa na theNkoromo Blog

2 comments:

  1. UONGOZI WA CCM MKOA WA KIGOMA,WAKIDHALILISHA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KUWADHALILISHA WATU ZAIDI YA MIAMOJA WAKIWEMO WANAUME,KINA MAMA WAJAWAZITO WATOTO WACHANGA NA WALEMAVU KWA KUWAFUNGIA VYUMBA MASAA TAKRIBANI 12 BILA RUHUSA YA KUINGIA NDANI KWAO NA FAMILIA MBILI KUCHUKULIWA VITU VYAO NA MAHITAJI YOTE YA KIBINADAMU NA KUWAACHA WAKILALA OVYO NA KUOMBAOMBA MISAADA YA KIUTU.PIA ASASI 2 ZIKIWA KATIKA WAKATI WA KUTEKELEZA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO KWA WANAJAMII ZIMEFUNGIWA VYUMBA VYAO NA KUCHUKULIWA VITENDEA KAZI VYOTE KINYUME NA UTARATIBU KWA FITINA ZA WATENDAJI TU NA UONGOZI MBAYA USIOJALI WALA KUONA HASARA YA WATU KUHANGAIKA HATA KAMA WANGEHAMA CHAMA.WAULIZENI KIGOMA HUO UONGOZI WA CCM UNAFANYAJE?KISA UPANGAJI TU KWENYE JENGO LA UWANJA WA LAKE TANGANYIKA ULIZENI WENZETU KUNA NINI?

    ReplyDelete
  2. UONGOZI WA CCM MKOA WA KIGOMA,WAKIDHALILISHA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KUWADHALILISHA WATU ZAIDI YA MIAMOJA WAKIWEMO WANAUME,KINA MAMA WAJAWAZITO WATOTO WACHANGA NA WALEMAVU KWA KUWAFUNGIA VYUMBA MASAA TAKRIBANI 12 BILA RUHUSA YA KUINGIA NDANI KWAO NA FAMILIA MBILI KUCHUKULIWA VITU VYAO NA MAHITAJI YOTE YA KIBINADAMU NA KUWAACHA WAKILALA OVYO NA KUOMBAOMBA MISAADA YA KIUTU.PIA ASASI 2 ZIKIWA KATIKA WAKATI WA KUTEKELEZA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO KWA WANAJAMII ZIMEFUNGIWA VYUMBA VYAO NA KUCHUKULIWA VITENDEA KAZI VYOTE KINYUME NA UTARATIBU KWA FITINA ZA WATENDAJI TU NA UONGOZI MBAYA USIOJALI WALA KUONA HASARA YA WATU KUHANGAIKA HATA KAMA WANGEHAMA CHAMA.WAULIZENI KIGOMA HUO UONGOZI WA CCM UNAFANYAJE?KISA UPANGAJI TU KWENYE JENGO LA UWANJA WA LAKE TANGANYIKA ULIZENI WENZETU KUNA NINI?

    ReplyDelete

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages