SHINYANGA, Tanzania
MKUU wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Wilson Khambaku amemsimamisha kazi mtendaji wa kata ya Bubiki tarafa ya Mondo anayetuhumiwa kuiba magunia 103 ya mahindi yaliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa kwa msaada wa kusaidia chakula kaya masikini kata hiyo.
Mkuu huyo aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Busangwa na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa kata hiyo,ambapo alitoa kauli ya mtendaji huyo aliyefahamika kwa jina la Boniface Charles ashitakiwe na kupelekwa mahakamani huku uchunguzi zaidi ukiendelea kwa wengine walioshirikiana nae.
Hatua ya kumsimamisha kazi na kuagiza akamatwe na kufikishwa mahakamani alisema kuwa tuhuma hiyo katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi kitengo cha upelelezi wilayani humo imeonekana mtendaji wa kata hiyo kuhusika kwa kushirikiana na baadhi ya watu wengine.
“Wananchi msiwe na wasiwasi tutawakamata tu,hatua zitakazochukuliwa na kamati ya maafa ya wilaya ni kuagiza uchunguzi ufanyike dhidi ya viongozi wasiokuwa waadilifu wanaohusika na upotevu wa mahindi ya msaada magunia 103 ikiwa kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika leo mtendaji huyo inaonekana anahusika.”alisema Nkhambaku.
Jeshi la polisi linaendelea kuwasaka wale wengine walioshirikiana na mtendaji wa kata ili nao waweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hiyo.
Mkuu huyo aliwahakikishia wananchi hao kuwa serikali ipo makini na kuwatoa hofu kwa kupata msaada wa mahindi mengine kama mgao ulivyopangwa ingawa tayari imeonekana kupata hasara dhidi ya upotevu wa mahindi hayo.
Baadhi ya wakazi waliohudhuria mkutano huo John Shija na Soseja Maduhu walisema kuwa mahindi ya msaada waliyaona yakishushwa katika ofisi ya kata lakini hawakuona yamegawiwa wapi kadri siku zinavyozidi kwenda huku kaya zikiendelea kulala na njaa na kufikiri mahindi hayo yalikuwa siyo yao bali yaliwekwa kuhifadhiwa.
Your Ad Spot
Oct 1, 2013
Home
Unlabelled
MTENDAJI KISHAPU, ADAIWA KUKWAPUA MAGUNIA 103 YA MAHINDI YA NJAA YALIYOTOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
MTENDAJI KISHAPU, ADAIWA KUKWAPUA MAGUNIA 103 YA MAHINDI YA NJAA YALIYOTOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇