LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 20, 2013

KINANA ATAKA WALIMU WATATULIWE KERO ZAO HARAKA

2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia waimbaji wa kwaya mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Nyashimo Wilayani Busega katika mkoa wa Simiyu, Ndugu Abdulrahman Kinana amemaliza ziara yake kwenye mkoa huo ambapo amekagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wenyeviti wa mashina pamoja na wanachama wa CCM ili kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi katika maeneo mbalimbali moani humo, Kinana anaaza Ziara ya siku sita katika mkoa wa Mara. Akihutubia katika mkutano wa hadhara leo uliofanyika mjini Lamadi Busega Kinana ametoa miezi sita kwa Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Serikali za Mitaa TAMISEMI Hawa Ghasiapamoja na watendaji wengine wa Serikali katika sekta ya Elimu kuhakikisha wanashughulikia kero za walimu hasa katika malipo yao mbalimbali ili kumaliza tatizo la malimbikizo hayo, Kinana amesema kama watendaji hao wa serikali hawatamaliza tatizo hilo atawashughulikia kwa kuwashitaki kwa wabunge wa CCM ili wawawajibishe kwa kukiuka agizo la Rais Dr.Jakaya Kikwete ambaye aliagiza watendaji hao kumaliza matatizo ya walimu, Katika picha katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Besega Ndugu Paul Mzindakaya na aliyenyanyua mkono kushoto ni Mbunge wa jimbo la Busega Dr. Titus Kamani. (PICHA NA KUKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-LAMADI SIMIYU) 1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye wakifurahia ngoma za akina mama walipowasili katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu. 9Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki kwa mwenyekiti wa kikundi cha waendesha bodaboda wa Nyashimo Gasper Mabula 7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimnawisha mikono Mwenyekiti wa shina Sina namba 1 kijiji cha cha Nyamatembe Bi. Sophia Kayenze tayari kwa kupata kifungua kinywa cha chai kwa Michembe . 5Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Busega Ndugu Paul Mzindakaya katika kijiji cha Nyamatembe. 4Nape Nnauye katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na wananyamitembe mara baada ya kuwasili kijijini hapo wakitokea Bariadi. 10Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa kama mshauri mkuu wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Kikwete katika kijiji cha Mwamanyiri mahari ambapo Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. nyerere alipumzika na kulala akitokea Butiama kwenda Mwanza wakati akiunga mkono Azimio la Arusha mwaka 1967. 14Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga ofisi ya Chama cha Mapinduzi kata ya Mwamanyiri huku Nape Nnauye akimsaidia kumpati tofari. 15Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika kata ya kabita wilayani Besega. 17Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki kwa mwenyekiti wa kikundi cha waendesha Lamadi Busega bodaboda Doto Paulo .21Mkuu wa mkoa wa Simiyu Ndugu Pascal Mabiti kulia akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Besega Paul Mzindakaya kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Lamadi Busega.20Kikundi cha ngoma cha lamadi Busega kikitumbuiza katika mkutano huo.23Wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa hadhara wakifuatilia matukio ya mkutano huo.24Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akuhutubia wananchi katika mkutano huo wa hadhara mjini Lamadi wilayani Busega. 25Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Lamadi Simiyu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages