- APONGEZA WANANCHI WA KATA YA NATTA KWA KUSHIRIKIANA
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mwalimu wa masomo ya sayansi Ndugu Silvester Joseph , Katibu Mkuu alitembelea shule ya Natta Secondary na kushuhudia jinsi masomo ya sayansi yanavyopewa kipaumbele.
Shule ya Natta inatumia Maabara inayotembea (Mobile Laboratory).
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wajasiriliamali wa kuendesha boda boda na ukulima wa mboga mboga mara baada ya kuzindua kikundi hicho ambapo aliwasihi lazima wapate elimu ya biashara wajue namna ya kuweka na kukopa na kulipa madeni kwa wakati.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka ndani ya ukumbi wa mkutano wa MUGUMU CCM ambapo alikutana na vijana wajasiriamali wa wilaya hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Natta mara baada ya kumaliza kikao na balozi wa shina namba 11 Tawi la Natta Majengo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa shukrani kwa wazee wa Natta baada ya kumpa heshima ya kuwa Mzee wa Natta.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇