LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 19, 2013

TRENI YA MWAKYEMBE YAIPATIA SERIKALI SH. MILIONI 3.5 KWA SIKU

NA BASHIR NKOROMO
SERIKALI inapata mapato ya takribani Sh. milioni 3.5 kwa siku kutokana na usafiri  wa treni katika jiji la Dares Salaam.

 Hayo  yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) Dk.Zacharia Mganilwa wakati  akimkabidhi tuzo Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe kwa mchango wake  mkubwa  wa kuboresha sekta ya reli  nchini kwa niaba ya kampuni  ya Mwandi Tanzania kwenye  hafla ya makabidhiano  iliyofanyika leo  jijini Dar es Salaam. 

Aidha Dk. Mganilwa tuzo pia imetolewa kutokana na  Waziri Mwakyembe ameweza kufufua na kuweka kwenye fikra Reli ya Musoma ya kwenda  Arusha na Reli Tanga.

Akizungumza katika makadhiano hayo,Dk.Mganilwa amesema  kuwa tuzo hiyo ilizingatia vigezo vyote muhimu vya  kumpata mshindi kwa kuzingatia mchango wa muhusika katika sekta ya  hiyo ,mtazamo wa wananchi kwa mtu husika na msimamo binafsi wa mtu husika kwenye uboreshaji  huo.

 “Ninyi ni mashuhuda wa mapinduzi ya usafiri wa treni za abiria jijini Dar es Salaam unaowanufaisha zaidi ya abiria 14,000 kila siku na ikumbukwe kwamba wazo la kuanzishwa usafiri huo lilikuwepo lakini Mheshimiwa Waziri ndiye aliyekuja  kufanya ndoto hiyo kuwa uhalisia”alisema Dkt.Mganilwa.

Tuzo hiyo imepatikana baada ya kushindanishwa kwa majina matatu ya watu ambao wana mchango mkubwa kwenye maendeleo na mapinduzi ya reli Tanzania kwa kurejea kila mmoja katika kipindi chake cha na kile alichokifanya.

Aidha ameiomba Serikali kupitia wizara ya hiyo kuanzisha mfuko wa miundo mbinu kwa fedha zitakazo kuwa zinapatikana katika usafirshaji ili kuweza kuendelea kuboresha suala hilo na  kukuza uchumi wa nchi yetu pamoja na kuleta maendeleo.

Naye Waziri Mwakyembe ameishukuru kampuni   hiyo kwa kuuona mchango wake katika jamii na kuweza kumpatia tuzo, ambayo  ni motisha   itakayo muongezea juhudi za kuliletea Taifa letu maendeleo kupitia sekta ya hiyo.

“Kwa niaba ya TRL, RHACO na wafanyakazi wote wa wizara ya Uchukuzi napenda kuishukuru kampuni  ya Mwandi Tanzania kwa kuuona mchango wangu katika sekta ya usafiri wa treni bado tunaendelea kuweka mipango madhubuti kuboresha usafiri wa treni nchini na Afrika Mashariki kiujumla”alisema Dkt.Mwakyembe.

 Watu  wengine walioshiriki katika ushindani wa tuzo hiyo, Injia Festo Mwanyika na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Reli  Tanzania na Linford Mboma kutoka   Shirika la Reli la Tanzania  na Zambia (TAZARA).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages