WASHINGTON, DC, Julai 22, 2013 – Benki ya Dunia imetoa changamoto kwa nchi za Afrika kuhimiza maendeleo endelevu ya ardhi ili kupunguza umaskini na kujiletea maendeleo. |
Ripoti
ya Benki hiyo iliyotolewa Julai 22, 2013
imeeleza kuwa ingawa nchi za Afrika ina karibu nusu ya eneo la ardhi
nzuri ambayo haijaendelezwa kwa kilimo,
bara hilo limeshindwa kuiendeleza ardhi
hiyoinayokadiriwa kuwa hekta milioni 202
kujikwamua katika umaskini, kuleta maendeleo ya uchumi,kuongeza nafasi za kazi
na kulleta mafanikio kwa jumla.
Ripoti
hiyo inayoitwa “Kutumia ardhi ya Afrika kwa mafanikio ya pamoja,”
inaeleza kuwa nchi za Afrika najamii
zake zinaweza kabisa kuondoa tatizo la uporaji wa ardhi, kuzalisha mazao ya
chakula na kubadilisha taratibu za
usimamizi na umiliki wa ardhi katika
mwongo ujao.Afrika,
Ripoti
hiyo imeeleza, ina kiwango kikukbwa cha
umaskini ambapo asilimia 47.5 ya watu
wake wana kipato chini ya dola za Marekani
$1.25 kwa siku..
“Licha ya kuwa na ardhi kubwa na utajiri wa madini, Afrika bado ni maskini ,” anasema Makhtar Diop, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika.
“Licha ya kuwa na ardhi kubwa na utajiri wa madini, Afrika bado ni maskini ,” anasema Makhtar Diop, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika.
“Kuboresha
usimamiaji wa ardhi ni muhimu kwa maendeleo ya haraka na kutoa nafasi zaidi kwa waafrika , wakiwemo wanawake ambao
ni asilimia 70 ya wakulima wa Afrika ambao wanakwazwa kumiliki ardhi na sheria za kimila..Hali
hii haikubaliki na lazima ibadilike ili waafrika waweze kunufaika na ardhi yao.”
Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi ya ardhi haijarasimishwa, hivyo kuwa na hatari kubwa ya uporaji na kuchukuliwa kwa malipo ya chini ya fidia.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi ya ardhi haijarasimishwa, hivyo kuwa na hatari kubwa ya uporaji na kuchukuliwa kwa malipo ya chini ya fidia.
Hata
hivyo kumekuwa na matumaini ya maboresho
chini ya mipango inayoendelezwa katika nchi za Ghana, Malawi, Msumbiji,, Tanzania, na
Uganda ambapo mpango wa
kutumia ardhi kwa mafanikio ya
pamoja unaweza kuleta mapinduzi ya
uzalishaji wa kilimo na uporaji wa ardhi na kuondoa umaskini wa kutupea Afrika..
Mpango wa kuleta mabadiliko
Ripoti hiyo inapendekeza kuwa Afrika inaweza kufanikiwa kuendeleza ardhi yake katika kipindi cha muongo ujao kwa::
· Kuwa na mabadiliko na uwekezaji kurasimisha ardhi na maeneo muhimu yanayomilikiwa na watu binafsi.
· Kusimamia taratibu za umiliki za maeneo yaliyovamiwa na kujengwa bila mpangilio mijini ambapo wanaishi zaidi ya watu asilimila 60 barani Afrika. .
· Kukabiliana na udhaifu wa utawala na rushwa katika mfumo wa usimamizi wa ardhi katika nchi za Afrika ambao kwa kawaida unapendelea wakubwa na kuathiri maslahi ya wananchi walio maskini.
· Serikali za Afrika kuwa na dhamira ya kisiasa kuhimiza mabadiliko haya ya ardhi kuvutia raslimali na uwezekezaji wa jamii ya kimataifa. .
Ripoti hiyo inasema kuwa mpango huo utagharimu nchi za Afrika na washirika wa maendeleo , ikiwemo sekta bianfsi kiasi cha dola za Marekani bilioni 4.5 katika kipindi cha miaka 10 kuleta mabadiliko ya sera na uwekezaji

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇